Kassim Majaliwa alizaliwa Disemba 12, 1960 katika Kijiji cha Nandagala Tarafa ya Nnacho wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi.
Alijiunga na Shule ya Msingi Mnacho mwaka 1970 hadi 1976 kabla ya mwaka 1977 hadi 1980 kupata elimu ya sekondari katika Shule ya Kigonsera alikotunukiwa cheti cha kuhitimu elimu ya sekondari (CSEE).
Baada ya kuhitimu elimu ya sekondari, Kassim alijiunga na Chuo cha Walimu Mtwara mwaka 1991 hadi mwaka 1993.
Mwaka 1994-1998 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa masomo ya Shahada ya kwanza kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Stockholm mwaka 1999 na kuhitimu mwaka huo huo.
Kazi
Majaliwa ni mwalimu kwa taaluma. Â Mwaka 1984-1986 aliajiriwa kama mwalimu katika Halmashauri ya Lindi na kati ya mwaka 1988 hadi 2000 aliajiriwa kama Mkufunzi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Mwaka 2001 alikuwa Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na mwaka 2001 hadi 2006 alikuwa Katibu wa CWT wa Mkoa kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi mwaka 2006 hadi 2010.
Siasa
Majaliwa aliingia katika siasa mwaka 2010 alipochaguliwa na wananchi kuwa Mbunge wa Jimbo la Ruangwa.
Akiwa Mbunge alichaguliwa na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kuwa Naibu Waziri wa OWM-TAMISEMI wadhifa ambao ameushika hadi alipongombea tena mwaka huu katika jimbo hilohilo na kuibuka mshindi.
Familia
Ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watatu na ana mke mmoja na watoto wanne.