29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

HUWEZI KUPENDWA NA MTOTO KAMA HUMPENDI

 

 

NA AZIZA MASOUD,

MARA nyingi watoto hugawanya  wazazi kihisia  kulingana na jinsi anavyompa uzito na upendo mzazi mmoja na kumwacha mwingine.

Upendo wa mtoto kwa mzazi fulani mara nyingi humuumiza mzazi mwingine   kihisia, mara nyingi watoto huwa wanakuwa wazi kujipambanua kihisia,  hivyo muhusika anajua hata kama asipoongea mbele za watu.

Tatizo hili halipo tu kwa watoto bali hata wazazi wapo ambao wanaoonyesha upendo moja kwa moja kwa mtoto fulani  kati ya watoto alionao kwa sababu ya kushindwa kuficha hisia zake.

Wapo ambao wanaweza kuwalea watoto wao kwa kuwaonyesha upendo sawa na kumpenda mtoto fulani bila kuweka wazi kwa wengine.

Katika familia  mara nyingi watoto hugawanyika kwa wazazi katika upendo, wapo ambao wanakuwa wanampenda baba na wengine watampenda mama  hilo ni suala la kawaida.

Upendo wa mtoto kwa mzazi husababishwa na ukaribu baina ya mtoto na mzazi  katika masuala mbalimbali.

Baadhi ya watoto  wanampenda mzazi fulani upendo wa kawaida kwa sababu ni mzazi wake na anamuona kila siku, mwingine anampenda kwa sababu anamjali.

Upendo wa  mtoto hujengwa  na hisia  jinsi unavyomchukulia na kutilia uzito baadhi ya mambo yanayomhusu  ndivyo na yeye atakavyoweza  kuonyesha mapenzi.

Zipo changamoto zinawakuta baadhi ya wazazi wanaofanya kazi  kwa sababu kutumia muda mrefu ofisini na kukosa muda wa kukaa karibu na watoto.

Wapo wazazi ambao wanafanya kazi lakini wanapendwa  na watoto kwa sababu  wanaishi kwa kuwajali, utakuta mtoto katika familia  kila kitu anamwambia baba au mama tu. Hii inatokana na mtu husika jinsi anavyomjali na kumchukulia.

Katika malezi ya watoto wapo wazazi ambao wanakosea na kudhani kuwa kuwatolea watoto ukali, kuwasema vibaya ni sehemu ya kutafuta heshima yake kama mzazi bila kujua kama anapaoteza upendo wake kwake.

Wazazi lazima tujifunze kupenda watoto, ni ngumu sana  kama utakuwa unamchukia yeye kurudisha upendo, lazima atakutengeneza kama sehemu ya adui hata bila kukwambia.

Pia kuna haja ya kuwaheshimu watoto, kuwasilikiza na kuheshimu hisia zao, endapo utaishi na mtoto kwa utaratibu huo hakuna atakayekuchukia wala kukuona mbaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles