23 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

HUSEA YAFURAHISHWA MIPANGO MIJI KUHAMISHIWA WIZARANI

 

Mwandishi Wetu, Wetu

Kampuni ya Mipango Miji na Vijiji inayotoa ushauri elekezi kuhusu ardhi (HUSEA), imesema imefurahishwa na hatua ya kuhamisha shughuli za Mipango Miji kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwenda Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Akizungumza na wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 13, Mwenyekiti wa kampuni hiyo Renny Chiwa amesema shughuli hizo zinapaswa kufanywa na wataalamu waliosomea mambo hayo ili waweze kubadilisha ramani ya miji.

“Kitendo cha wanasiasa kuingilia kati kinachangia kurudisha nyuma maendeleo ya nchi Kwa sababu na wenyewe wanakuja na ramani zao ambazo hazikidhi viwango.

“Shughuli za mipango miji zinapaswa kufanywa na watalaamu walisomea mambo hayo ili kuweka ramani za miji ambazo zitakidhi viwango Kwa miaka 20 ijayo, kwa hilo tunampongeza Rais John Magufuli kuliona suala hilo na kulifanyia kazi, amesema Chiwa.

Amesema uamuzi wa rais ni kutaka kuboresha shughuli za mipango miji pamoja na kuwawajibisha watendaji ambao watashindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo ambapo kutokana na hali hiyo mabadiliko hayo yanaweza kuleta tija na nchi kuwa na mipango bora ya ardhi itakayotoa sura mpya.

“Kimsingi wataalamu wa ardhi na mipango miji katika halmashauri ni sawa na watumishi wengine katika serikali za mitaa, kwa sababu wamekuwa wakiwajibika Tamisemi moja Kwa moja, hivyo basi kurudishwa wizarani kutasaidia kuwapa fursa ya kutumia taaluma zao katika kubadili mandhari ya jiji,” amesema.

Wiki iliyopita Rais Magufuli aliagiza watalaamu wote wa ardhi na mipango miji katika halmashauri zote nchini kusimamiwa moja kwa moja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,305FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles