27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Hukumu ya Zitto yaibua mjadala

 KULWA MZEE -DAR ES SALAAM

UAMUZI wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumtia hatiani Kiongozi wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa uchochezi na kumuhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja kwa masharti, umeibua mjadala kuhusu hatma yake kisiasa.

Zitto amepewa masharti ya kutotamka wala kuandika kauli zenye uchochezi mitandaoni kwa muda wa mwaka mmoja.

Maeneo hayo mawili tayari yameibua mjadala mkubwa kuhusu hatma yake kisiasa lakini pia iwapo atajizuia kunyamaza au kuandika na kuzungumza jambo lolote litakalo weza kutafsiriwa na mamlaka kuwa ni uchochezi.

HUKUMU YAKE

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alisema upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 15 na kwamba wameweza kuthibitisha mashtaka bila kuacha shaka yoyote.

“Maneno yaliyotamkwa na Zitto ni magumu, makali na hayakuwa na ukweli wowote kwani yalishindwa kuthibitishwa kwenye utetezi.

“Ni maneno ambayo hayana ushahidi wa kutosha, hakuna palipothibitishwa kwamba askari wamemuua nani na ushahidi unaonesha tukio lilifanyika alfajiri muda ambao huwezi kusema nani alimuua nani “ alisema Hakimu Shaidi

“Maneno yalikuwa ‘strong’ maneno serious watu 100 kufa sio kitu kidogo hadi kutaja watu wa kabila fulani, ni sawa na kuwasha moto kwenye nyasi kavu,” aliongeza.

“Jamii ina watu wenye uelewa tofauti na uwezo wa kuchuja maneno hivyo kila mmoja anaweza kuchuja maneno kwa kadri anavyoweza,”. 

Baada ya maelezo hayo alisema mahakama imejiridhisha kuwa Zitto ana hatia katika makosa yote matatu aliyoshtakiwa nayo,”alisema.

Mawakili walipotakiwa kuzungumza lolote kabla ya adhabu, Wakili wa Serikali Renatus Mkude alisema mshtakiwa ni mkosaji kwa mara ya kwanza lakini aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali ili

 iwe fundisho kwa wengine wenye tabia ya kutoa kauli za uchochezi.

Wakili wa utetezi, Steven Mwakibolwa aliiomba mahakama isitoe adhabu kali kwa kuwa mshtakiwa ana familia inayomtegemea, ni baba wa watoto wanne na hana rekodi za jinai kwenye mahakama. 

Aliomba mahakama hiyo impe adhabu ya faini.

Hakimu Shaidi baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili alisema imezoeleka sasa watu kusema Mahakama ya Kisutu imegeuka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) huku akisisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda amani ya nchi.

Hakimu Shaidi alisema mahakama inamtia hatiani na inamuhukumu kifungo cha nje mwaka mmoja kwa masharti ya kutotamka wala kuandika kauli zenye uchochezi mitandaoni kwa muda wa mwaka mmoja.

Inadaiwa Oktoba 28, 2018 katika Makao Makuu ya ACT-Wazalendo, Kijitonyama jijini Dar es Salaam Zitto alitamka”…watu ambao walikuwa ni majeruhi katika tukio la mapambano baina ya wananchi na Polisi wakiwa wamekwenda hospitali kupata matibabu katika kituo cha afya Nguruka, Polisi wakapata taarifa kuwa kuna watu wanne wamekwenda hospitali kituo cha afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua..’’

Katika mashtaka ya pili ilidaiwa Oktoba 28, 2018 maeneo ya Kijitonyama katika Makao Makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam, alitoa maneno ya uchochezi dhidi ya Jeshi la Polisi akisema ‘’…lakini tumefuatilia kwa kina jambo hili, taarifa ambazo tumezipata kutoka kijijini Mpeta-Nguruka, Uvinza ni mbaya, ni taarifa ambazo zinaonesha wananchi wengi sana wameuawa na jeshi la Polisi pamoja na kwamba afande 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles