23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 22, 2023

Contact us: [email protected]

Hukumu’ ya mahekalu Dar kesho

lukuvi*Kesi ya kupinga bomoabomoa kunguruma mahakamani leo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

HUKUMU ya nyumba za kifahari (mahekalu) zilizojengwa sehemu zisizoruhusiwa, inatarajiwa kuanza kutekelezwa kesho kama ilivyotangazwa na Serikali.

Hatua hiyo, inatokana na Serikali kusitisha bomoabomoa kwa kipindi cha wiki mbili, ili kutoa fursa kwa wakazi wa maeneo ya mabondeni kuhama na kutangaza kuwa zoezi hilo litaanza tena Januari 5, mwaka huu.

Miongoni mwa nyumba ambazo zimezua gumzo, ni ile inayomilikiwa na Mchungaji wa  Kanisa la Assemblies Of God, Dk. Getrude Lwakatare.

Nyumba hiyo, imewekewa alama ya X  na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) ikidaiwa kuwa ipo katika hifadhi ya bahari.

Serikali ilikwishatoa agizo la utekelezwaji wa Sheria ya Mipango Miji ya Mwaka 1979, inayokataza wananchi kuishi maeneo hayo na kujenga ndani ya mita 60 kutoka kwenye hifadhi ya bahari.

Mwanasheria wa Mchungaji huyo, Jerome Msemwa, ameitaka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kuheshimu  hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam  juu ya uhalali wa kuwapo  kwa nyumba hiyo.

Alisema kwa mujibu wa hukumu hiyo, Mchungaji Lwakatare ana haki ya kuendelea kuishi eneo hilo, bila ya kusumbuliwa na mamlaka yeyote juu ya kitendo cha bomoabomoa.

“Kuna watu wameweka alama ya X inayotaka nyumba ya mchungaji kubolewa, huku wakiwa hawatambui kufanya hivyo ni kupingana na hukumu ya Makahama Kuu iliyomruhusu kuendelea kuwapo hapo kwa sharti la kutojenga ndani ya mita 60,” alisema.

Kwa mujibu wa Msemwa hukumu hiyo ilitolewa Mei 21, mwaka jana na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ikimtaka mchungaji huyo kutojenga ndani ya mita 60 ya hifadhi ya bahari.

Uamuzi huo, ulitangazwa na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ambaye alisema alisitisha ubomoaji kwa siku 14 kwa wakazi wa maeneo husika  kuondoa vitu mbalimbali vilivyopo katika maeneo yao.

Ubomoaji nyumba zilizopo jirani na Mto Msimbazi ulianza Desemba 17, mwaka huu ambapo hadi sasa nyumba zilizovunjwa ni 353 katika jiji la  Dar es Salaam pekee.

Alisema kazi hiyo, inafanywa  na wizara yake kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

“Eneo la Mto Msimbazi ni hatarishi, kufanya ujenzi wowote katika eneo hilo ni kinyume na Sheria ya Mipango Miji Namba 8 ya mwaka 2007 na Sheria ya Mazingira Namba 4 ya mwaka 2004,” alisema Lukuvi.

Lukuvi pia alisema wananchi hawaruhusiwi kubadili matumizi ya ardhi kinyume na taratibu zilizoainishwa kwenye Sheria ya Mipango Miji Namba Nane ya mwaka 2007, Kifungu cha 30 na Waraka wa Kitaalamu Namba Moja wa mwaka 2006.

“Baadhi ya maeneo yaliyovamiwa jijini Dar es Salaam upande wa Kinondoni ni 111, Ilala 50, Temeke ni 19, tunaziomba mamlaka zote za upangaji nchini, zitekeleze agizo la kuwaondoa wavamizi katika maeneo yaliyoainishwa

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,020FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles