22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

HUDUMA ZA USAFIRI ZAZIDI KUWA KIDIGITALI ZAIDI

Na Mwandishi Wetu


USAFIRI wa Uber ni wa gharama nafuu na salama zaidi ukilinganisha na usafiri mwingine hapa nchini. Usafiri huu ni wa kutumia magari madogo yanayoweza kubeba kuanzia mtu mmoja hadi wanne.

Gharama zake huanzia Sh 3,000 na kuendelea kulingana na mahali unakokwenda, watu wengi wanaufurahia kwa kuwa hata inapotokea wamesahau kitu ndani ya gari hukipata kikiwa salama.

Ili biashara iweze kukua zaidi, ushirikiano ni jambo muhimu. Kwa sababu hii, Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo na Uber wameamua kuingia makubaliano ya kibiashara ili kuwaondolea usumbufu wateja wao.

Ushirikiano huu wa kimkakati ulisainiwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, ukilenga kuwasaidia watumiaji wa Uber kufanya malipo ya safari zao kupitia Tigopesa, moja kati ya mifumo maarufu ya malipo ya kidigitali nchini.

Gharama za kuita taxi pia hazitakuwapo kwa watumiaji wa Tigo, hili ni jambo la kupongeza zaidi.

Ushirikiano huu unahakikisha miamala ya malipo isiyo na usumbufu kwa watumiaji wa Uber ambao hawana kadi za malipo za bank (Credit au Debit card), ambao pia wanahitaji urahisi wa miamala isiyo ya fedha taslimu.

Wateja zaidi ya milioni sita wanaotumia huduma ya Tigopesa tayari wanalipa bili za huduma mbalimbali na nyinginezo kwa kutumia Tigopesa.  Watakuwa pia na fursa ya kupata Uber kwa haraka na kwa usalama zaidi, usafiri wa uhakika pamoja na huduma nyinginezo.
Ushirikiano huu wa kwanza wa aiana yake kwa Uber Afrika Mashariki, ni hatua kubwa ya safari ya Tanzania kuelekea mapinduzi ya kidigitali na ni maono ya Tigo ya kuwa na maisha ya kidigitali yenye werevu na yanayounganisha huduma mbalimbali ambayo wakati wote imekuwa ndio kauli mbiu ya Tigo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari anasema ushirikiano kati ya Uber na Tigo utaleta huduma mpya kwa wateja wao pamoja na Uber jijini Da es Salaam.

“Tunapongeza athari nzuri za mabadiliko katika teknolojia ya simu nchini. Ushirikiano wetu na Uber utahamasisha kutumia mitindo mipya ya kipekee ya maisha ya kidigitali katika soko hili linalokua kwa kasi, ikiwa inapanua utumiaji wa Uber na Tigo kwa mamililoni ya Watanzania,” anasema Karikari.
Wakazi wa jijini Dar es Salaam wanawakaribia kwa kasi wenzao wa Jiji la Nairobi, nchini Kenya katika kuingia katika biashara ya Taxi inayoshamiri.

Kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, Uber imekua na kufikisha magari 3000 jijini Da es Salaam kukiwa na uwezekano wa kupanuka kuelekea katika maeneo mengine ya Tanzania.

Meneja wa Uber Afrika Mashariki, Loic Amado anasema ushirikiano huu unadhihirisha nia ya dhati ya kampuni kuwahudumia wasafiri, madereva kwa upana zaidi kupitia mbinu halisi za hapa nchini.

“Ushirikiano huu unawakilisha msingi muhimu kwa ajili ya sisi kufanya mapinduzi ya usafiri wa taxi hapo baadae,” anasema Amado.

Naye Meneja wa Uber nchini, Alfred Msemo anasema madereva na watumiaji wa Uber watavuna matunda ya biashara yatokanayo na ushirikiano huu.

“Tunashauku kuhusu ushirikiano wetu na Tigo nchini Tanzania, ambao utasaidia watumiaji wote wa Uber na madereva wenye line za Tigo kutumia App ya Uber katika simu zao bure bila malipo yoyote.  “Uber ni App ya Smartphone ambayo husaidia kuwatoa watu kutoka sehemu A kwenda sehemu B kwa kubofya kitufe.  “Wito na maono ya Uber ni kutoa huduma ya usafiri ambayo ni salama, ya uhakika na yenye gharama nafuu kwa kila mtu, kila mahali. Ushirikiano huu utahamasisha maelfu ya wakazi wa Dar es Salaam ambao ni wateja wa Tigo kutumia App ya Uber kuzunguka sehemu mbalimbali hapa jijini,” anasema Msemo.

Kampuni hizi mbili zitakuwa zikifanya kazi kwa pamoja katika bidhaa na promosheni ambazo zinalenga kuongeza thamani kwa wateja wapya na waliopo.

Tigo na Uber nchini Tanzania watatangaza ofa za kusisimua hivi karibuni kuwasaidia wateja kuwasiliana na Uber jijini Dar es Salaam ambako huduma za usafiri huo zinapatikana kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles