27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

‘HUDUMA ZA MOCHWARI HAZIJAPANDA MUHIMBILI’

NA VERONICA ROMWALD-DAR ES SALAAM


HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), imesema  gharama inazotoza kulipia huduma ya kuhifadhi maiti haijapanda.

Kauli hiyo imetolewa baada ya baadhi ya ndugu wa marehemu ambao hufikisha wagonjwa hao na kukutwa na  mauti hospitalini hapo, kulalamikia kupanda kwa gharama kimyakimya.

Akizungumza na MTANZANIA mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja Muhimbili, Aminiel Aligaesha,  alisema huwa wanatoza kiasi cha Sh 30,000 pekee kwa siku.

“Majokofu yetu ni ya kiwango cha hali ya juu, yana uwezo wa kuhifadhi mwili wa marehemu hata mwaka mzima pasipo kuharibika.

“Hii ni Hospitali ya Taifa, gharama hizi tunatoza kwa kipindi cha miaka sita sasa na hazijabadilika sijui watu kwa nini wanalalamika,” alisema.

Alisema huwa wanatoza gharama hizo kwa ajili ya kuchangia ununuzi wa umeme.

Alisema hata hivyo gharama hizo huweza kuongezeka iwapo ndugu wa marehemu watapenda kupatiwa huduma nyingine ikiwamo ile ya kusafisha maiti.

“Sisi tunawajibika kuhifadhi mwili wa marehemu na kutoza fedha hizo kuchangia umeme na matengenezo kama yatahitajika kufanyika.

“Lakini kama ndugu watapenda mwili uoshwe na au kurembwa basi hizo ni gharama nyingine ambazo watawajibika kuzilipa kulingana na huduma waliyopewa,” alisema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,608FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles