22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Huduma msaada wa kisheria kuendeshwa kidigitali

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAM

HAKI ni sehemu ya maisha ya mtu ya kila siku na ni muhimu kuhakikisha huduma za upatikanaji wa haki  zinapatikana kwa karibu na urahisi kwa jamii.

Lakini kama ilivyo katika sekta nyingine, ni dhairi kwamba sekta hii muhimu kwa kiasi kikubwa pia imeathirika na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala alieleza kuhusu maeneo ya utekelezaji wa mradi wa ‘Access to Justice’ yanavyoathiriwa na ni jinsi gani changamoto hizi zimeleta fursa ya kujikita kiteknologia.

Alisisitiza ni muhimu kwa wadau mbalimbali kutafuta njia mbadala katika kutekeleza shughuli zao ili kuwawezesha wananchi kuendelea kupata haki zao.

Alisema Legal Services Facility imekuwa ikiwawezesha wasaidizi wa kisheria zaidi ya 3,700 nchini kuwafikia wananchi kila wilaya na kutoa elimu ya kisheria na kutatua changamoto zao. 

Lulu alisema watoa huduma hao wamekuwa wakitoa elimu kwenye mikutano mikubwa ya hadhara, mabonanza, vikoba, mashuleni, katika sehemu za ibada na maeneo mengi yenye mkusanyiko wa shughuli ambazo kwa sasa hazifanyiki kutokana na mlipuko wa corona.

Akizungumzia kuhusu ushirika wa watoa huduma wa msaada wa kisheria  katika masuala ya Covid-19, Mkurugenzi Mkuu wa Morogoro Paralegal Centre (MPLC), Flora Masoy alisema; “MPLC  ilituma maombi kwa Kamati ya Covid-19 ya Mkoa inayosimamiwa na Katibu Tawala ili ‘paralegal’ (wasaidizi wa kisheria) wetu wapate mafunzo  juu ya maswala  ya corona na pia walifundishwa jinsi ya kutengeneza vitakasa mikono. 

“Lengo kubwa lilikuwa ni kuwawezesha ‘paralegal’ kutoa elimu kwa wananchi namna ya kujikinga na corona.

“Mafunzo haya yalifanyika na sasa ‘paralegal’ wanatoa elimu hii kwa jamii kwa kushirikiana na halmashauri na watoa huduma wa afya wa wilaya.” 

Lulu alisema janga la corona limeambatana na changamoto na ukiukwaji wa haki za binadamu kwa namna mbalimbali, ikiwemo haki za usalama, uhai, elimu, afya, na uhuru wa kutembea popote utakapo kutokana na hatua muhimu ambazo serikali imechukua kulikabili tatizo hili.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,502FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles