HUDDAH: NINA PESA, NAISHI NITAKAVYO

0
541

NAIROBI, KENYA

MWANAMITINDO mwenye vituko vingi nchini Kenya, Huddah Monroe, amesema haogopi kufanya lolote kwa ajili ya maisha yake kwa kuwa anaamini hawezi kumfurahisha kila mtu.

Alisema anapata kiasi kikubwa cha fedha kinachomwezesha kufanya chochote anachotaka kwa ajili ya maisha yake na si kila wanalotaka watu wengine.

“Ninaingiza kiasi kikubwa cha fedha, naishi nitakavyo na nafanya nitakacho na siwezi kamwe kufanya anachotaka shabiki, ila ushauri kwa shabiki fata mazuri yangu na mabaya yangu niachie mwenyewe.

“Siwezi kumfurahisha kila mtu bali najifurahisha mwenyewe kwa ninachoona kizuri kwangu kwa kuwa sifanyi vya watu, bali ni vyangu na haya ndiyo aina ya maisha ninayoyataka,” aliandika Huddah.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here