26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

WAZIRI ATAKA WATOTO WALIOUNGANA KAGERA WAFIKISHWE MUHIMBILI HARAKA

Na Mwandishi wetu               |         


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, kuhakikisha watoto waliozaliwa wakiwa wameungana wanafikishwa Muhimbili.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo leo bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo ambaye alihoji je serikali ina taarifa kuwa kuna watoto wamezaliwa Kagera wakiwa wameungana.

Akijibu swali hilo, Ummy amesema: “Wanaozaliwa wakiwa na maumbile ya ajabu wapelekwe hospitali.

“Na kuhusu watoto waliozaliwa wakiwa wameungana huko Kagera, namwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera ahakikishe watoto hao wanafikishwa Muhimbili,”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles