24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

MAPACHA WALIOUNGANA CONSOLATHA, MARIA WAFARIKI DUNIA

Na Mwandishi Wetu          |


Mapacha walioungana Maria na Consolatha Mwakikuti, wamefariki dunia leo usiku Juni 2, katika Hospitali ya Serikali mjini Iringa.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amethibitisha kufariki kwa mapacha hao baada ya kupata taarifa za mapacha hao kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ambaye hata hivyo hakupatikana kwenye simu.

“Nimepata taarifa za kufariki kwa mapacha hao na nimesikitishwa sana na taarifa hizo, ni watoto ambao walikuwa na bidii katika masomo yao na walikuwa na matumaini ya maisha lakini Mungu amewapenda zaidi,” amesema.

Hata hivyo, Kasesela amesema amewasiliana na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo amesema atatoa taarifa za mapacha hao kesho asubuhi.

“Hospitali na nyumbani kwangu si mbali, tumekwenda kuwaandaa na kuwahifadhi katika chumba cha maiti, Mganga alikuwa anapigiwa simu nyingi sana kuhusiana na kifo cha watoto hao ameona ni busara atoe taarifa kesho,” amesema Kasesela.

Februari mwaka huu, mapacha hao Maria na Consolatha, walilazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), walikuwa wakisoma Chuo Kikuu cha RUCO mjini Iringa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,853FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles