LONDON, England
BAADA ya idadi kubwa ya makocha kuhusishwa na kibarua cha kuinoa Newcastle United, hatimaye klabu hiyo imemtangaza Eddie Howe.
Howe (43), ambaye anachukua nafasi ya Steve Bruce aliyefukuzwa hivi karibuni, amekuwa nje ya kazi ya ukocha tangu alipotemana na Bournemouth mwishoni mwa msimu wa 2019-20.
Mwanzoni mwa mwaka huu, Howe alifuatwa na mabosi wa Celtic ya Scotland lakini alikataa ofa yao, huku Newcastle ikitolewa nje na Unai Emery aliyesema anataka kubaki Villarreal.
Akizungumzia kupewa ulaji huo, Howe amesema: “Ni heshima kubwa kuwa kocha wa klabu yenye historia kama Newcastle United. Ni siku ya kujivunia kwangu na familia yangu.”