23.9 C
Dar es Salaam
Thursday, September 29, 2022

‘HOUSE BOY’ AMCHINJA MTOTO WA BOSI WAKE KISA KUMUOMBA MUA

Raymond  Minja, Iringa

Jeshi la polisi mkoani Iringa, linamshikilia mfanyakazi wa ndani wa kiume, kwa tuhuma za kumchinja mtoto wa bosi wake kisa kuombwa kipande cha mua alichokuwa anakula mfanyakazi huyo.

Mtuhumiwa huyo, Gofrey Joshephat (29), mkazi wa Ipogolo, anadaiwa kumuua kwa panga mtoto huyo na kisha kuuweka mwili wake kwenye kiroba na kwenda kuutupa kwenye pagale jirani na nyumbani kwao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire amesema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo jana Julai 4, saa nane mchana maeneo ya Kobwabwa B, Manispaa ya Iringa.

“Siku ya tukio mtuhumiwa alikuwa nyumbani na marehemu nyumbani akila mua ambapo marehemu alimuomba mtuhumiwa kipande cha mua, alipokataa mtoto huyo alimtolea mtuhumiwa lugha ya kuudhi ndipo alipochukua panga na kuanza kumkata shingoni na mikononi na kuchukua kisu na kumchinja na kisha kwenda kumtupa kwenye pagale,” amesema.

Aidha, Kamanda Bwire amesema bado jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ikiwamo kumpeleka mtuhumiwa huyo kwa wataalamu kumpima kama ana akili timamu kiasi cha kumuua mtoto kisa kumuomba mua.

Mtoto huyo amezikwa jana katika makaburi ya familia huko Kibwabwa, Manispaa ya Iringa.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,298FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles