HOTUBA YA UPINZANI YAKWAA KISIKI BUNGENI

0
633

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Naibu Spika, Dk. Tulia Akson leo amewagomea Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuwasilisha taarifa ya kudumu ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kutokana na kutowasilisha taarifa yao kwa Spika siku moja kabla ya kusomwa bungeni.

Kwa mujibu wa waraka wa Spika, taraifa za kuwasilishwa bungeni zinatakiwa kuwasilishwa kwa Spika siku moja kabla ya siku kuisoma bungeni.

Dk. Tulia amesema waraka wa Spika ulitolewa kutokana na siku za nyuma baadhi ya taarifa kusomwa bungeni wakati hazipo kwenye kiti wala wabunge hawajapatiwa.

“Kutokana na hali hiyo, hotuba ambazo zimefika mezani kwa Spika ni ya Waziri Mkuu na kamati za Bunge pekee na ndiyo zitakazosomwa,” amesema Naibu Spika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here