26.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Hospitali zatakiwa kuwa na ICU za watoto

NA  MWANDISHI WETU – PWANI

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu ameziagiza hospitali za rufaa nchini kuwa na wodi maalumu za wagonjwa mahututi  (ICU) kwa ajili ya watoto wachanga ili kupunguza vifo vyao.

Waziri Ummy alisema hayo jana wakati akikagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.

Alitoa agizo mbele ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ambapo alimtaka ahakikishe watoto wachanga lazima wawe na ICU yao ili kuhakikisha vifo vya watoto wachanga vinapungua nchini.

“Watoto wachanga ambao ni wagonjwa, wawena ICU yao, lengo letu kama Serikali ni kupunguza vifo vya watoto wachanga, kwasababu tukipunguza vifo vya watoto wachanga,  tutakuwa tumepunguza vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano,”  alisema WaziriUmmy.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa karibu 40%  ya vifo vya watoto ni watoto wachanga na katika kila watoto 100, watoto 40% ni wachanga, hivyo Serikali inaendelea kuchukua jitihada za makusudi ili kupunguza vifo hivi, ikiwemo kusisitiza kila hospitali nchini kuwa na ICU.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,424FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles