24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Hospitali ya Mirembe yaongeza muda wa kutoa huduma

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

HOSPITALI ya Taifa ya Afya ya Akili, Mirembe, imefanya mabadiliko katika utoaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa nje, ambapo muda wa kuanza kutoa matibabu ni saa moja asubuhi badala ya saa mbili asubuhi.

Lengo la uongozi wa hospitali kufanya mabadiliko hayo ni kuboresha huduma za afya ili kuwezesha watu mbalimbali kupata huduma za matibabu mapema zaidi na kwa wakati.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Dk. Paul Lawala, alisema mabadiliko hayo yanahusu huduma zote za afya, ikiwamo huduma za afya ya akili pamoja na magonjwa ya mwili.

Dk. Lawala alisema tangu kuanza kwa utekelezaji wa mabadiliko hayo,  kumekuwapo na matokeo chanya kwa kuwa watumishi wamefurahia kuanza kutoa huduma mapema, huku wagonjwa na ndugu wakifurahia utaratibu mpya wa kupatiwa huduma mapema na kurejea nyumbani mapema.

“Matokeo chanya yameanza kuonekana kwani watumishi wameitikia wito wa kuwahi mapema na kuanza kutoa huduma saa moja asubuhi.

“Hatua hii imesaidia watu kupata huduma za matibabu mapema na kwa wakati na pia watu wengi wamevutiwa na mabadiliko haya,” alisema Dk. Lawala.

Naye Mkuu wa Kitengo Cha Wagonjwa wa Nje, Dk. Isack Mrimi, aliwataka wananchi kufika katika  hospitali hiyo kupata huduma za matibabu kwa kuwa Mirembe ina wataalamu wabobezi wenye uwezo wa kutoa huduma bora na kwa wakati.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles