Nairobi,Kenya
Waziri wa Afya nchini Kenya, Mutahi Kagwe ametoa ripoti ya uhaba mkubwa wa mitungi ya Oksijeni katika Hospitali kadhaa nchini humo kufuatiwa ongezeko la idadi kubwa la wagonjwa wa Corona.
Ripoti hiyo iliyotolewa na Waziri kagwe siku ya Jumatatu machi 29 na kutoa wito kwa wananchi wa Kenya wanaotumia mitungi hiyo katika hospitali za watu binafsi, Sekta pamoja na majumbani kuzirudisha kwa watengenezaji ilikutumika katika hospitali zenye uhitaji.
Pia alisema mahitaji ya soko la Oksijeni yameongezeka zaidi ya mara mbili ya awali kutoka tani 410 kabla ya janga la ugonjwa wa Corona hadi kufikia tani 880 kwa sasa.
Nchi ya Kenya imethibitishwa kuwa na wagonjwa wa corona 130,000 na vifo zaidi ya watu 2,000.