27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Hospitali Kuu Lugalo yazindua idara ya kusafisha figo

Na  AVELINE  KITOMARY

DAR ES SALAAM

HOSPITALI Kuu ya  Jeshi  Lugalo, imezindua rasmi  idara  mpya ya kusafisha figo (dialysis), baada ya idara hiyo kubuniwa na kutekelezwa na jeshi hilo ili kuboresha huduma za matibabu.

Jengo hilo lililogharimu zaidi ya Sh milioni 431 na vifaa vyake vikigharimu Sh milioni 633, inalenga kupunguza gharama za matibabu kwa wanajeshi na wananchi wenye matatizo ya figo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi huo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Husein Mwinyi alihimiza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuendelea kuwa kitovu cha ubunifu,utekelezaji na usimamizi mzuri wa rasilimali na huduma zinazoanzishwa ndani ya jeshi hilo.

“Uzinduzi wa idara hii, ni wakati muafaka kwa wakati huu  magonjwa ya figio yanaongezeka, majeshi na wananchi wanauhitaji mkubwa, nimpongeze mkuu wa majeshi bila shaka itakuwa msaada mkubwa ndani ya nchi na Serikali inaendelea kuongeza huduma za afya moja wapo, ni hii ya Lugalo huduma bora zitapatikana nalipongeza jeshi.

“Mradi huu, umebuniwa na kutekelezwa na jeshi hii inaondoa dhana ya utegemezi kama iliyojengeka,tujifunze kutumia ubunifu tulionao.

Dk.Mwinyi alitoa wito kwa madaktari na wauguzi wa hospitali kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa wananchi kwa kufata taratibu na maadili waliyofundishwa

“Nitoa wito kwa  jeshi ambao  wanaendelea kutoa huduma kwa wananchi wote,waendelee kutoa ushirikiano huduma zote zinawanufaisha wote.

“Na pia wahudumu wa afya wawe na lugha zenye faraja, kwani lugha nzuri  ni dawa kwa wagonjwa,o ni muhimu kufata maadili ya kazi ili hata wananchi na wanajesahi waweze kufurahia huduma mnazotoa,”alishauri Dk. Mwinyi.

Katika hatua nyingine, aliipongeza Serikali kuendelea kupanua na kuongeza huduma za afya hapa nchini na kupunguza gharama za kufata matibabu nje ya nchi.

“Sasa wanajeshi hawatahitaji kwenda kwingine,Serikali itaacha kutumia gharama kubwa kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi na kufanya fedha hizo ziende kwenye kazi zingine za maendeleo.

“Naipongeza Serikali  kutoa fedha kwa ajili ya mradi huu wa teknolojia ya hali ya juu, ni mradi wa gharama, nawaasa utumike kwa uangalifu mkubwa kutumia kama rais anavyosema tuwe makini na kutunza vifaa,”alisema Dk.Mwinyi.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo  aliishukuru Serikali kwa miongozo bora kwa kuhakikisha jeshi linapiga maendeleo katika huduma zote zinazohitajika.

“Hospitali hii ni moja ya huduma bora ndani ya nchi, fedha zilitolewa na rais mwaka 2017 leo hii tumekusanyika kusimamia uzinduzi kwahiyo huduma hii ni ya heshima kwani katika kipindi kirefu wanajeshi walikuwa wanatibiwa hospitali ya umma na nje ya nchi lakini sasa huduma hiyo itapatikana hapa.

“Na gharama zitapungua,utegemezi katika Hospitali ya Muhimbili umesababisha msongamano lakini leo hii tunayofuraha kupata huduma hii hapa na Muhimbili msongamano utapungua.

“Ujenzi ulianza mwaka 2016 na kukamilika mwaka 2017, baada ya hapo tukaanza kutafuta mashine hizi zimetoka nchini Ujerumani na zimeanza kufanyiwa majaribia kwa wanajeshi wetu waliosomea,”alieleza Mabeyo.

Naye Mkuu wa Hospitali  hiyo na daktari bingwa wa masikio, pua na koo, Brigedia Jenerali Gabriel Muhize  alisema sasa kupitia idara hiyo wanaweza kuwahudumia wagonjwa 10 kwa wakati mmoja na gharama za matibabu zinatarajiwa kushuka kulingana na ukubwa wa tatizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles