25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Hospitali Kagera kusafisha damu wagonjwa wa figo

Nyemo Malecela -Kagera

HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera inatarajia kuanza kutoa matibabu ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo ifikapo Novemba.

Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Museleta Nyakiroto, alisema huduma hiyo inatarajiwa kuanza mwishoni mwa Novemba, baada ya kupokea mashine tano za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo kutoka wizarani.

“Wataalamu kutoka kampuni iliyoleta hizo mashine tayari wameshafika, wameshaandaa eneo zitakapokaa na wametoa maelekezo ya nini kifanyike.

“Tumeshapanga bajeti na kuwapatia majina ya watumishi watakaopatiwa elimu ya kuzitumia hizo mashine,” alisema Dk. Nyakiroto.

Alisema hospitali hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa ambao figo zao zimeshindwa kufanya kazi wasiopungua watano kila mwezi.

“Wagonjwa hao tulikuwa tukiwapeleka katika hospitali ya Bugando mkoani Mwanza,” alisema.

Wakati huo huo, Dk. Nyakiroto alisema pia hospitali hiyo imepata mashine ya digitali ya x-ray ambayo ilitolewa na wizara.

“Kabla ya kupata x-ray hiyo, tukuwa na x-ray mbili za analogi ambazo zimekuwa zikiharibika mara kwa mara na kusababisha hospitali kuingia gharama za kutengeneza,” alisema.

Alisema mashine ya kisasa imerahisisha kazi kwa wahudumu wa afya, kwani imesaidia usafirishaji wa picha za wagonjwa kutoka katika x-ray moja kwa moja kwenye kompyuta za madaktari na kuzalisha picha zenye ukubwa wa wastani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles