25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

HONGERA DIAMOND KWA KUTAMBUA MCHANGO WA WANAHABARI

NA MWANDISHI WETU

VYOMBO vya habari vinashika nafasi za juu katika kumkuza msanii mwenye kipaji ili sanaa anayofanya iwafikie watu wengi. Wasanii wote wakubwa duniani wenye mafanikio wamepita kwenye magazeti, redio, runinga na tovuti mbalimbali zilizowakutanisha na mashabiki sahihi ambao ni wanunuzi wa kazi zao.

Msanii anapaswa kuwa na uhusiano mzuri na vyombo vyote vya habari ili anapotoa kazi mpya au anapokuwa na onyesho, wanahabari wafanye kazi yao ya kuwafahamisha mashabiki.

Wasanii wakubwa duniani waliochuja kisanaa kuna nyakati walikosana na vyombo vya habari kwa kuwakosea heshima, kuwapiga au kuwavunjia vifaa vya kazi wanahabari.

Wakati akijiandaa kuwasha mitambo ya kituo chake cha runinga, nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, jana alionyesha kutambua umuhimu wa wanahabari na vyombo vya habari vilivyochangia kwa kiasi kikubwa mafanikio yake kwenye muziki.

Ni ukweli usiopingika kuwa, vyombo vya habari kama vile magazeti, redio, runinga, tovuti zimesimama nyuma ya mafanikio yake kwa kutangaza muziki anaofanya na mambo mengine yanayohusu umaarufu wake wenye tija katika sanaa anayofanya.

Lakini pia vyombo vya habari vimekuwa vikimkosoa pale anapokosea na kufanya aenende kwenye njia iliyonyooka, hivyo kuyavuta mafanikio yaliyokuwa mbali naye kipindi anaanza safari yake ya muziki miaka zaidi ya 8 iliyopita.

Sasa amepata mafanikio na kuamua kuwekeza kwenye tasnia ya habari ili runinga na redio yake iungane na vyombo vya habari vingine kusaidia chipukizi wanaohitaji msaada wa wanahabari  ili wapae kisanaa, hii ni hatua nzuri na kubwa kuwahi kufanywa na msanii wa Tanzania.

Katika maelezo yake aliyoyatoa jana, Diamond Platnumz alisema sababu kubwa iliyomsukuma kufanya hivyo ni kutoa ajira kwa vijana ambao wengi wao ni waandishi wa habari, watangazaji, Djz, wanafunzi wa shule na vyuo na kukuza sanaa kwa kusaidia wasanii chipukizi.

Mwimbaji huyo aliendelea kukiri kuwa, licha ya kuwa ni msanii aliyepiga hatua fulani kwenye sanaa, anaamini ana deni kubwa kwa jamii na wanahabari, ndiyo maana kwa sehemu yake ameamua kuanzisha runinga na redio ili kupunguza deni hilo.

Hili ni jambo kubwa linalopaswa kuigwa na wasanii wengine, kwani ni vyema kukumbuka walipotoka, ili kutengeneza mazingira mazuri ya kuishi vyema nyakati zao za kutamba zitakapopita.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles