Honeymoon kufanya kazi na waigizaji wa Nigeria

0
832

NA MWANDISHI WETU

LICHA ya kutoka kapa katika hafla ya tuzo za Africa Magic Viewers Choice 2016 zilizofanyika Lagos nchini Nigeria, mwongozaji bora wa filamu katika tuzo za ZIFF, Honeymoon Mohammed, amesema mipango yake ya sasa ni kufanya filamu pamoja na wasanii wenye majina makubwa kutoka nchini Nigeria.

HoneymoonHoneymoon aliwataja wasanii anaotarajia kufanyanao kazi akiwemo, Ginevieve ni Van Viker, Don Dimelo, Blossom Chukwujekwu na Tope Tedela.

“Kwa filamu wenzetu wa Nigeria wametuzidi na hawana maringo kama wasanii wetu hapa, nimeshangaa nilipozungumza na mastaa hao walionyesha nia ya kushirikiana nami wengi walivutiwa na picha za filamu zangu wakaniambia wanataka kufanyakazi nami jambo ambalo kwa waigizaji wa Tanzania huwa ngumu kutokana na kujivuna,” alisema Honeymoon.

Honeymoon aliongeza kwamba, kushirikisha wasanii hao kutasaidia kuongeza hamasa ya kutimia kwa lengo lake la kutaka kutengeneza filamu itakayokuwa na waigizaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

“Nataka kutengeneza filamu ya Afrika ambayo tutaunganisha waigizaji mbalimbali kutoka kote Afrika maana ili filamu iwe ya Afrika inabidi wasanii washiriki watoke nchi mbalimbali za Afrika ndivyo navyotaka kufanya,’’ alieleza Honeymoon.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here