29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Home Shopping Centre yafunga biashara zake

1NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Home Shopping Centre imefunga biashara zake zilizokuwa jijini Dar es Salaam na katika mikoa mingine.

Tangazo la kampuni hiyo yenye maduka yanayouza bidhaa mbalimbali za nyumbani na ofisini, lilitolewa jana katika ukurasa wa 20 wa gazeti la Daily News la nchini likisema imevunjwa kwa hiari.

“Umma unafahamishwa kuwa kupitia azimio maalumu la Oktoba 5, mwaka huu, Home Shopping Centre Limited imeamua kuivunja kampuni kwa hiari,” limesema tangazo hilo.

Kadhalika tangazo hilo limesema kuwa Yusufu Mohamed kutoka Kampuni ya uwakili ya Law Domain ya jijini Dar es Salaam, ndiye aliyeteuliwa kuwa mfilisi kwa madhumuni ya kuivunja kampuni hiyo.

“Wadai wote wa kampuni wanatakiwa kumpatia mfilisi maelezo ya kutosha ya madai yao dhidi ya kampuni hiyo ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hilo,” lilisema tangazo hilo.

Julai, mwaka juzi, mmiliki wa Home Shopping Centre, Said Mohammed Saad, alimwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana na kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Tukio hilo lilitokea karibu na Kituo cha Polisi cha Oysterbay kilichopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles