28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

HOMA YA MAFUA YA NDEGE YAGUNDULIWA UGANDA

philippines_tubbataha_9_teri_aquino

Kampala, Uganda

 SERIKALI  ya Uganda, imethibitisha kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya mafua ya ndege katika maeneo ya Entebbe, Masaka magharibi mwa mji wa Kampala  na fukwe za Ziwa Victoria.

Wizara ya Kilimo nchini humo imesema virusi hivyo vimethibitika kuwapo kwa bata na kuku wanaofugwa.

Majaribio yaliyofanywa na wataalamu katika maeneo mawili ikiwemo ufukwe wa Ziwa Victoria, yalithibitisha kuwa, ndege hao walifariki kutokana na maradhi ya Highly Pathogenic Avian Influenza au bird flu, yaani homa kali ya ndege kama inavyofahamika.

Chembechembe zilizokusanywa kutoka kwa mizoga ya bata wa kufugwa na kuku, katika wilaya moja ya eneo hilo karibu na Ziwa Victoria upande wa Uganda, zilithibitisha hilo.

Hakuna taarifa zozote za ugonjwa huo kuambukiza binadamu na Serikali ya Uganda imesema, inawashauri jamii za maeneo hayo kuhusu namna ya kujikinga kupatwa na ugonjwa huo na mbinu za kuzua kusambaa zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles