27.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Homa pambano la Yanga, Medeama chini

yanga

NA WINFRIDA NGONYANI, DAR ES SALAAM

HOMA ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kati ya wenyeji Medeama na Yanga imeonekana kuwa chini ukilinganisha na ilivyokuwa nchini Algeria, wakati Yanga ilipotua kucheza na Mo Bejaia.

Yanga tayari imetua Ghana katika mji unaoitwa Tarkwei, ambako mchezo huo utachezwa, kilomita 300 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Accra ambapo walitumia saa 5 hadi kufika huko.

Timu hizo zitavaana kesho katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika, mchezo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.
Akizungumza kwa njia ya simu nchini Ghana, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema hali ni tofauti kabisa nchini humo, kwani hakuna shamra shamra zozote kwa wenyeji, hasa mashabiki.
“Algeria ambako tulikwenda kuvaana na Mo Bejaia kulikuwa na mbwembwe nyingi kwa mashabiki, lakini Ghana kupo kimya utafikiri hakuna mechi.

“Kupo kimya sana, mchezo huu umekuwa hauzungumzwi na wakazi, hali ambayo unaweza kusema si ya kawaida, hatuoni mashabiki wakiwa na hamasa kama tulivyozoea kuona tukienda kucheza nchi nyingine,” alisema Saleh.

Alieleza hali hiyo haiwafanyi waone utakuwa ni mchezo usio na mashabiki wengi, bali watahakikisha wanapambana na kuibuka na ushindi, ili kujiweka kwenye matumaini ya kusaka nafasi ya kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

“Mchezo huu ni muhimu zaidi kwetu, licha ya kucheza ugenini na kila mchezaji amepewa maagizo na kocha kuhakikisha anafanya kile alichowaagiza,” alisema.

Waamuzi kutoka nchini Morocco watachezesha mchezo huo ambao ni mwamuzi wa kati Redouane Jiyed, akisaidiwa na Mohamed Lahmidi na Hicham Ait Abbou watakaoshika vibendera.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles