30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

HOLLANDE ADAI ANA WAJIBU WA KUTORUHUSU USHINDI WA LE PEN

PARIS, UFARANSA


RAIS wa Ufaransa anayeondoka madarakani Francois Hollande amesema jukumu lake kuu la mwisho ni kuzuia ushindi wa kiongozi wa chama cha National Front (NF), Marine Marie Le Pen katika uchaguzi mkuu wa mwezi ujao.

Holland alisema mgombea huyo wa chama hicho chenye siasa kali za mrengo wa kulia, huenda akashinda duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais itakayofanyika Aprili 23.

Wakati akiapa kufanya kila awezalo kwa kutumia madaraka yake kuhakikisha Le Pen hashindi urais, pia alionya matokeo ya uchaguzi mkuu yataamua si tu hatma ya Ufaransa, bali ya Umoja wa Ulaya (EU).

Kura za maoni zinaonyesha Le Pen atashinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo.
Wakati huo huo, mgombea urais wa chama cha kihafidhina, Francois Fillon, anayekabiliwa na kashfa ya kumlipa mkewe na wanawe mishahara kwa kutumia fedha za umma kwa kazi hewa, ameapa hakuna atakayemlazimisha kuondoka katika kinyang’anyiro cha kuwania urais.

Aidha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ufaransa, Alain Juppe, alisema hatochukua nafasi ya Fillon ya kugombea urais iwapo mgombea huyo atajiuzulu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles