26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

HOJA ZA MNYIKA ZAMVUTA SPIKA KUKALIA KITI

Na Elizabeth Hombo       |     


Hoja za Mbunge wa Kibamba, John Mnyika leo katika hali isiyo ya kawaida zimemfanya Mwemyekiti wa Bunge, Hajma Giga kumpisha kwenye kiti Spika Job Ndugai baada ya kuibuka mivutano baina ya wabunge wa upinzani na kiti wakati Mnyika akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha.

Hali hiyo ilijitokeza wakati Mnyika alipoanza kusema Wizara ya Fedha imekuwa ikitoa kauli zenye utata na kueleza kuwa kutokana na hilo, amemtaka Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango ili asiwe Waziri wa fedheha ni vyema akajiuzulu.

“Naibu Waziri wa Fedha wakati akitoa ufafanuzi kuhusu zilipo Sh trilioni 1.5 ambazo hazijulikani zilizo, alisema bilioni 209 zimepelekwa Zanzibar, lakini nimefuatilia mjadala wa Baraza la Wawakilishi hakuna ilipoonyeshwa zilipo hizo fedha,” amesema Mnyika.

Wakati akiendelea kuchangia, amesema uchunguzi ufanyike kuhusu taarifa kutolewa tofauti kuhusu deni la taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles