26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

HOJA YA NAPE YAMLIZA WAZIRI KAMA MTOTO

Na MAREGESI PAUL-DODOMA


HOJA ya Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM), aliyoitoa Mei 16, wakati Bunge likijadili Bajeti ya Wizara ya Kilimo, imemfanya Waziri wa wizara hiyo, Dk. Charles Tizeba, kulia kama mtoto wakati akijitetea mbele ya Kamati ya Bunge ya Bajeti.

Katika hoja yake, Nape alishika shilingi ya mshahara wa waziri wakati Bunge lilipoketi kama kamati kupitisha bajeti hiyo, akihoji sababu za Serikali kutorudisha kwa wakulima fedha za kodi inayotozwa kwenye korosho wakati wa kusafirisha nje zao hilo (export levy), kama ambavyo sheria inataka.

Nape alisema kutokana na kutorudishwa kwa fedha hizo, bei ya dawa za kupulizia mikorosho zimepanda maradufu na sasa ndiyo wakati wa kupuliza dawa hizo vinginevyo zao hilo litavamiwa na wadudu.

Kutokana na hoja hiyo kuungwa mkono na wabunge wengi wa CCM na upinzani, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu, aliyekuwa akiongoza kikao hicho, aliamuru suala hilo lipelekwe kwenye Kamati ya Bajeti ili lipate ufumbuzi.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles