25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Hofu yatanda United kumkosa Maguire

MANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa timu ya Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, ameweka wazi kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kuikosa huduma ya beki wao wa kati Harry Maguire kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Manchester City, kesho kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 27, amepata tatizo la enka ambalo linaweza kumfanya awe nje ya uwanja kwa siku kadhaa.

Nyota huyo wa timu ya taifa England, msimu huu amecheza jumla ya michezo 39 kwenye michuano mbalimbali tangu alipojiunga akitokea Leicester City mwishoni mwa msimu uliopita.

Juzi mchezaji huyo alikuwa nje ya uwanja kwenye mchezo dhidi ya Derby County kwenye michuano ya Kombe la FA kutokana na kusumbuliwa na nyama za paja, wakati huo timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Kocha Solskjaer ameweka wazi kuwa, wana wasiwasi ya kumkosa mchezaji huyo kwenye derby yao katika Uwanja wa Old Trafford, Jumapili hii.

“Nilifanya mazungumzo na mchezaji huyo juzi kabla ya kufanya mazoezi ya mwisho, nikamwambia lazima awe kwenye kikosi cha kwanza, lakini wakati wa mazoezi akapata tatizo la enka, hivyo ninaamini atakuwa nje ya uwanja, labda anaweza kurudi viwanjani mwishoni mwa wiki inayofuata,” alisema kocha huyo.

Hata hivyo, mchezaji huyo alitumia ukurasa wake wa Twitter na kuelezea jinsi gani alivyoumia kuukosa mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Derby County, lakini akadai atakuwa sawa muda mfupi ujao.

“Nimejisikia vibaya kuukosa mchezo dhidi ya Derby County, nilifanya mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo, lakini ni mipango ya mungu sikuweza kuwa sawa, ila ninaamini kila kitu kitakuwa sawa,” alisema mchezaji huyo.

Baada ya kumkosa mchezaji huyo kwenye mchezo wa juzi, kocha Solskjaer aliamua kuwatumia Victor Lindelof na Eric Bailly kwenye safu ya ulinzi, hivyo wachezaji hao wanaweza kutumia kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Manchester City.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,540FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles