30.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Hofu yatanda Pakistan na India kuingia vitani

ISLAMABAD, PAKISTANI

MGOGORO wa kidiplomasia kati ya nchi za India na Pakistan jana ulionesha dalili za utulivu baada ya Pakistan kuikabidhi India rubani wake aliyekuwa amekamatwa, Kamanda Abhinandan Varthaman, lakini hofu inaendelea kutanda wakati kukiwa na juhudi za mataifa yenye nguvu duniani za kuepusha vita kati ya majirani hao wawili wenye silaha za nyuklia. 

Kamanda Varthaman, alivuka mpaka na kuingia India muda mfupi kabla ya saa tatu kamili usiku juzi katika tukio la ngazi ya juu lililoonyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni. 

Mashambulizi ya kila upande kwenye mpaka wa jimbo linalogombaniwa la Kashmir yaliendelea hata baada ya kuachiwa kwake na kusababisha vifo vya watu wanne, lakini yakasitishwa usiku. Jeshi la Pakistan limesema leo kuwa vikosi vya angani na majini vinaendelea kuwa katika hali ya tahadhari. 

Mataifa yenye nguvu yakiwemo China na Marekani yametoa wito wa kujizuia ili kuepusha mgogoro mwingine kati ya nchi hizo jirani ambazo zimekuwa vitani mara tatu tangu zilipopata uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1947.

Kwa upande wake India imesema kuwa itaendelea kuipa shinikizo Pakistan kwa kile ilichokiita kuwa mzalishaji wa magaidi na kupanga njama za matukio ya kigaidi licha ya kuachiliwa huru kwa Kamanda Varthaman.

Serikali ya India imeituhumu Pakistan kufadhili kikundi cha ugaidi cha Jaish-e-Mohammad (JeM) ambacho kinatajwa kuhusika katika shambulizi la kigaidi la Februari 14 mjini Kashmir na sasa kimekuwa chanzo cha mgogoro katika mpaka wa jimbo hilo. 

“Kumwachilia huru Kamanda ni mipango ya India, bila makubaliano yoyote mezani. Hatukutaka kuona tukio hili likiwa kama lile la Kandahar likitokea kwetu. Kurejea kwa Kamanda Varthaman, haina maana kuwa India italegeza msimamo wake, bali tunataka kukitokomeza kikundi cha kigaidi kinachofadhiliwa na Serikali ya Pakistan.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan, amejaribu kuzungumzia mgogoro huo kwa lugha ya kidiplomasia zaidi yenye nia ya kuleta maelewano, tofauti na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, ambaye ametoa matamshi makali dhidi ya jirani zao hao.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,424FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles