24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Hofu ya kimeta yatua nchini

ngombeJOHANES RESPICHIUS -Dar es Salaam

WIZARA ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imesema ugonjwa ulioua watu wawili na wengine wanane kulazwa katika Hospitali ya Enduleni ndani ya Mamlaka Hifadhi ya Ngorongoro unaweza kuwa ni kimeta.

Hayo yalibainishwa   Dar es Salaam jana katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo, Dk. Maria Mashingo.

Alitoa taarifa hiyo siku mbili baada ya kuripotiwa kuwa ugonjwa wa sotoka umeua watu wawili na wanane kulazwa.

“Ugonjwa huo uliripotiwa kwa makosa, ambao umesababisha athari za  afya ikiwamo vifo vya watu wawili na wanane kulazwa hospitalini unaweza kuwa ni kimeta ambao ndiyo ugonjwa wa wanyama unaoathiri binadamu na upo maeneo ya Wilaya ya Ngorongoro.

“Wananchi wasiwe na hofu juu ya kuwahudumia mbuzi na kondoo wenye ugonjwa wa sotoka kwa vile  hauna madhara yoyote kwa afya ya binadamu.

“Ugonjwa wa sotoka kwa ng’ombe unajulikana kama ‘rinderpest’ na kwa mbuzi na kondoo unajulikana kama ‘Peste Des Petirs Ruminants’ (PPR) hivyo sotoka ya ng’ombe nchini tulishaitokomeza,” alisema Dk Maria.

Aliwataka wananchi kuchukua tahadhari ya kula nyama iliyokaguliwa na wataalamu wa mifugo na kuthibitishwa kuwa ni salama kwa matumizi ya binadamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles