30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Hofu ya corona; kampuni yaamuru wafanyakazi wake kufanyia kazi nyumbani

Uingereza

Kampuni ya mafuta nchini Uingereza, Chevron Corporation imelazimika kuwaamuru jumla ya wafanyakazi wake 300 kufanyia kazi zao nyumbani kwa muda ili kujiepusha na maambukizi ya virusi vya corona.


Hatua hiyo imekuja baada ya mfanyakazi mmoja kutoa taarifa ya kuwa na dalili za mafua.


Wafanyakazi hao wametakiwa kusubiri hadi uchunguzi utakapokamilika ili kubaini iwapo mfanyakazi mwenzao huyo ana virusi hivyo au la.


Msemaji wa kampuni hiyo amesema wanaendelea kufuatilia hali hiyo kwa ukaribu wakifuata mwongozo wa mamlaka za afya za kimataifa na kitaifa.


Amesema jukumu lao la msingi kama kampuni ni afya na usalama wa wafanyakazi wao na kwamba wamechukua hatua za tahadhari kupunguza hatari ya kupata maambukizi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles