25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

HIVI KWANI UJINGA NI NINI WANANGU?

Na RAMADHANI MASENGA

OOOIII, niaje masela? Kila kiungwa flengwa au mnabung’aa bung’aa tu? Shtuka bongo lala tumebadili mwendos siku hizi. Ukijifanya unajua sana kutembea wenzako watakupita kwa sababu wanakuja wakikimbia. Ama nini? Sana tu wanangu.

Dawa ya fasta sindano, sasa unapewa sindano unalia nini? Kausha ikuingie vema. Nashangaa kuna baadhi ya masela walitaka joto ya fasta, sasa wamesogezewa jiko karibu wanasema linaunguza sana. wadau wanasema njia ya peponi ina miba mingi, sasa kama unataka kula raha za paradiso inaidi tu uvumilie mbigiri miguuni.

Au sio? Acheni masikhara, mwacheni dereva aongeze kasi. Si ndiyo sisi tuliosema hatutaki gari la kusukuma tunataka la mwendo kasi. Sasa mnalalamika nini kwamba mnarushwa rushwa katika mashimo. Kumbe mlitaka mvua ila mliogopa radi. Acheni utoto wanangu.

Vaa mkanda kama kanali Sadali. Ujinga ni kutamani kufika peponi bila kufa. Ama ujinga ni nini wanangu? Binti unatamani kupata mtoto ila unaogopa mimba. Tikisa bichwa lako hilo kama liko sawa wewe.

Pepo haiji bila kifo na dhahabu haing’ai bila kupita katika moto. Tulia uungue ili baadaye uwe komando mwanangu. Pambana acha uzoba. Si ndiyo sisi tuliosema kwamba dereva yule  mwingine anasumbuliwa na mbavu hivyo safari yetu ilikuwa imejaa mashaka? Kwani ujinga ni nini wanangu?

Ujinga ni kuongea kitu bila kujua maana yake ila ujinga mkubwa ni kuimbishwa nyimbo bila kuelewa kiitikio chake.

Wanangu mtaji mkubwa ni fikra zako. Sasa wewe bung’aa kindezi.  Ruhusu bla bla za wanasiasa ndiyo ziwe maisha yako. Eti unaamini utakuja kuwa bosi kwa kukaa tu maskani nakupiga porojo.

Ujinga ni kuamini wanasiasa wana mbinu za miujiza za kukupa maendeleo bila kufanya kazi kwa bidii na maarifa. Bila kuminyika, kutoa jasho hata ikibidi damu kiduchu jua hukamati ngawira.

Sasa wewe endelea kupaka losheni za  kina dada pamoja na pafyumu zao kwa kuamini maisha yana kanuni za kukupendelea wewe. Piga kazi wewe.  Mwili wako ni juamba la utumwa la akili yako.

Uache utumike vizuri kwa malekezo ya akili yako ili baadaye uweke heshima mjini. Sasa wewe jione mjanja kulala masaa kumi na mbili. Sio tu unavaa hereni za dada yako kutaka nawe uonekane mjanja ila utaazima hadi lini nguo za dada zako.

Dunia hii ina maajabu yake masela. Sasa wee endelea kuona napoteza muda hapa. Ujinga ni kuamini niko hapa kwa ajili ya kukuchekesha.

Funua ubongo wako ule maarifa kutoka kwa Profesa wa kitaa na mkufunzi wa ghetto. Wanangu mmenisoma au mlikuwa mnasoma tu? Hahahaha!

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles