Hispania wafanya uchaguzi wa bunge

0
371

MADRID, HISPANIA

Raia wa Hispania wapatao milioni 37 wanapiga kura kulichagua bunge jipya kwa mara ya pili mwaka huu.

Kulingana na maoni ya raia, chama cha Kisoshalisti nchini Hispania (PSOE) cha Waziri Mkuu aliye madarakani, Pedro Sanchez kinaweza kupata tena kura nyingi.

Lakini Sanchez pia hatarajiwi kupata wingi wa kura wa kumwezesha kuunda Serikali, hali itakayoendeleza mkwamo wa kisiasa nchini humo.

Kwa miezi kadhaa Sanchez hakufanikiwa kuunda Serikali ya mseto, kufuatia kura ya mwisho mnamo mwezi Aprili, na kumfanya Mfalme Felipe VI kuitisha uchaguzi mwingine.

Kulinganana waangalizi, mojawapo ya mambo ambayo yalitarajiwa kushawishi uchaguzi wa jana Jumapili ilikuwa ni maandamano ya Catalonia kufuatia hukumu ya kifungo cha jela kwa viongozi tisa wa vuguvugu la kugombania uhuru wa jimbo hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here