Hillary: Sina tatizo kubwa la kiafya

0
1150

hillary-clintonWASHINGTON, MAREKANI

MGOMBEA urais wa Marekani kupitia Chama cha Democratic, Hillary Clinton, amesema hakuficha taarifa za kuugua homa ya mapafu kwa kuwa hakudhani kama litakuwa jambo kubwa na la kusumbua.

Amekuwa akikosolewa kwa kushindwa kutoa taarifa zake mapema hadi pale alipokaribia kuanguka mbele ya hadhara katika siku ya kumbukumbu ya shambulizi la Septemba 11.

Akihojiwa na Shirika la Habari la Marekani (CNN), Hillary alisema hakufuata vyema kile anachokiita ushauri wa madaktari wake wa kupumzika kwa siku tano baada ya kufanyiwa vipimo Ijumaa iliyopita.

Timu yake ya kampeni imesema kuwa hana tatizo lolote la kiafya, isipokuwa homa ya mapafu na kuongeza kuwa taarifa zaidi juu ya uimara wa afya yake zitatolewa.

Mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump, alisema kuwa anatumaini Hillary atapona hivi karibuni, na kuongeza kuwa ugonjwa wa mgombea huyo ni tatizo katika mbio za urais.

Trump alisema kuwa ofisi yake itatoa taarifa yake ya kiafya wiki hii.

Hillary alionekana kudhoofu kiafya siku ya kukumbukumbu ya watu waliofariki katika shambulio la Septemba 11, na aliondoka katika eneo hilo kwa msaada maalumu wa walinzi wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here