KLABU ya Chelsea imeanza kumfukuzia mshambuliaji wa Napoli, Gonzalo Higuain ambaye anaweza kuchukua
nafasi ya Diego Costa wakati wa dirisha dogo la usajili Januari mwakani.
Klabu hiyo imefanya maamuzi hayo baada ya kuona kwamba mchezaji wao huyo amekuwa na matukio mbalimbali ambayo hayaisaidia timu hiyo.
Kutokana na hali hiyo Costa ametakiwa kubadilika ili kuweza kuisaidia timu hiyo ambayo kwa sasa imekuwa na wakati mgumu katika michuano ya Ligi Kuu nchini England.
Hata hivyo, mchezaji huyo alikuwa na mchango mkubwa msimu uliopita ambapo aliipa ubingwa klabu hiyo huku
akiifungia mabao 20 ya Ligi Kuu baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea Atletico Madrid.
Kamati ya usajili ya klabu hiyo tayari imeanza kufanya mazungumzo na Higuain mwenye umri wa miaka 27
kwa ajili ya kuisaidia timu hiyo mzunguko wa pili.