25.8 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

HECHE ANG’ANG’ANIWA POLISI, KUFIKISHWA MAHAKAMANI KESHO

Na Leonard Mang’oha, Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia Mbunge wa Tarime Vijini, John Heche (Chadema), kwa tuhuma za kushindwa kuripoti polisi kama alivyotakiwa jeshi hilo.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitishwa kushikiliwa kwa mbunge huyo.

Mambosasa amesema Heche alikamatwa kwa kosa sawa na lile lililokuwa likimkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, ambaye pia alishindwa kuripoti polisi wiki iliyopita baada ya kwenda Afrika Kusini kwa matibabu kabla ya kukamatwa Uwanja wa Ndega wa Dar es Salaam (JNIA), usiku wa kuamkia juzi.

Aidha, Mambosasa amesema endapo taratibu zitakamilika mbunge huyo anaweza kufikishwa mahakamani kesho, kuunganishwa katika kesi ya viongozi wengine wa chama hicho waliopata dhamana leo.

“Ni kama alivyoshikiliwa mwenzake Mdee naye hakuripoti, walikuja wakatakiwa kurudi wote wao hawakurudi, hakuna kosa jipya kosa lake ni kutorudi hadi wenzake wanapelekwa mahakamani,” amesema Mambosasa.

Machi 27 mwaka huu Heche alishindwa kuripoti polisi pamoja na viongozi wengine saba wa chama hicho kama walivyotakiwa na jeshi hilo akidai alikuwa na msiba.

Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ambao wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwamo kuhamasisha maandamano, uchochezi na uasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles