27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Hazina yaongeza mishahara ya Rais Uhuru, msaidizi wake

NAIROBI, KENYA

HAZINA imeongeza malipo ya mishahara kwa Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Rais William Ruto kwa asilimia 3.9 baada ya awali kupunguzwa mwaka 2017.

Nyaraka za Hazina zimeonesha malipo ya jumla kwa mwaka; mshahara na posho — ya  Kenyatta na Dk. Ruto yatapanda kutoka ya sasa milioni 36.6 za Kenya hadi Sh milioni38, ambazo ni sawa na Sh bilioni 720 za Tanzania,

Awali malipo ya watendaji hao wakuu wa umma ilkatwa pamoja na ya maofisa wengine wa ngazi ya juu, kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 8, 2017 ili kukabiliana na mzigo wa bajeti ya mishahara.

Hilo lilishuhudia mshahara wa rais ukipungua hadi Sh milioni 1.44 kwa mwezi kutoka Sh milioni 1.65 sawa na Sh milioni 33 za Tanzania, wakati naibu wake akipokea Sh milioni 1.23 kutoka Sh milioni 1.4za Kenya sawa na Sh milioni 28 za Tanzania.

Uamuzi huo wa hazina unakuja huku ikitekeleza mpango wa kubana matumizi ili kupata fedha za shughuli za maendeleo pamoja na kugharimia huduma muhimu kama usalama, afya na elimu.

Serikali inakabiliwa na changamoto ya kushindwa kufikia malengo ya makusanyo ya mapato na kusababisha ukosefu wa fedha ulioufanya Hazina kupitia upya bajeti yake.

Wakati huo huo, wabunge nao wanapania kujiongezea malipo ya kugharimia ofisi zao za mikoani ifikapo Julai mwaka huu, huku spika wa bunge la taifa akiunga mkono mapendekezo hayo.

wabunge wamejipangia malipo ya Sh bil 7.9 za Kenya sawa na Sh bil.194 za Tanzania kugharamia maandalizi ya afisi zao za mikoani, kadhalika malipo ya wasaidizi wao kuanzia Julai mwaka huu.

Tume ya kuwaajiri wabunge, PSC, inasaka ridhaa ya watunga sheria kuiongeza bajeti yao ya operesheni kwa shilingi milioni 440. Kwa sasa wabunge wamtengewa shilingi bilioni 6.8.

Spika wa bunge la taifa aliye pia mwenyekiti wa PSC, Justin Muturi, anaunga mkono mapendekezo hayo.

Tayari wabunge wanapewa mkopo wa gari usiotozwa kodi, hela ya usafiri, malipo ya uzeeni na kadhalika posho za kuhudhuria vikao vya kamati za bunge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles