24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Hazard aonesha jeuri ya fedha Madrid

MADRID, HISPANIA

MSHAMBULIAJI mpya wa timu ya Real Madrid, Eden Hazard, ameonesha jeuri ya fedha kwenye Wilaya ya La Finca mjini Madrid kwa kununua mjengo wenye thamani ya pauni milioni 10, ambazo ni zaidi ya bilioni 27 za Kitanzania.

Lengo la kununua nyumba hiyo ni kutaka kuishi na familia ikiwa pamoja na mama yake baada ya kukamilisha uhamisho wake wa kitita cha pauni milioni 150, akitokea Chelsea wakati huu wa kiangazi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ameamua kununua nyumba kwenye wilaya hiyo ambayo inadaiwa kuwa na wachezaji wenzake wengi wa timu ya Real Madrid.

Ramani ya nyumba hiyo ilitengenezwa na mkali wa majengo Joaquin Torres, ikiwa na vyumba sita ambapo Hazard akiwa na mke Natacha, watoto watatu wa kiume Yannis, Leo na Samy pamoja na mama yake.

Mbali na kuwa na vyumba sita, ndani ya nyumba hiyo kuna bwawa la kuogelea (Swimming pool), chumba cha kuunyoosha mwili, chumba cha mazoezi (gym), chumba cha Sinema na uwanja wa kuchezea tenisi nje ya nyumba hiyo.

Hazard mbali na kujiunga na timu hiyo katika maandalizi ya msimu mpya wa ligi, bado hakuonesha moto wake huku akidaiwa aliongezeka mwili kutokana na kutumia muda mwingi kuwa na familia yake wakati wa mapumziko mara baada ya kumalizika kwa msimu wa Ligi England.

Hata hivyo, kwa mujibu wa uongozi wa timu hiyo, umeweka wazi kuwa Hazard ameanza kurudi kwenye kiwango chake na wanatarajia makubwa kutoka kwake hasa kwenye michuano ya Ligi Kuu nchini Hispania ambapo mchezo wa kwanza Real Madrid watatupa karata yao leo dhidi ya Celta Vigo ambapo utakuwa mchezo wao wa ufunguzi huku ikiwa tayari Ligi hiyo imefunguliwa tangu jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles