23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

HAYA NI MAGONJWA SUGU KWA WACHEZAJI

Na ZAINAB IDD – DAR ES SALAAM


TANZANIA imebarikiwa kuwa na idadi kubwa ya wachezaji wenye vipaji na uwezo, lakini wengi wao wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa ya mara kwa mara ambayo kwa namna moja au nyingine hupelekea wengi wao kushindwa kutimiza ndoto na kujikuta wakitumikia viwango vyao kwa muda mfupi.

Jambo la kawaida kusikia mchezaji akiuguza majeraha kwa muda mrefu na kukaa nje kwa kipindi kirefu.

Ulimwenguni kote wachezaji wa soka wamesikika wakisumbuliwa na majeraha ambayo yamekuwa sugu na mwisho huishia kuhatarisha vipaji na maisha yao.

SPOTIKIKI ilifanya mahojiano na Katibu wa Chama cha Madaktari wa Michezo nchini (TSMA), Nassoro Matuzya, ambaye alieleza kuwa magonjwa sugu yanayowaandama wachezaji kila mara ni matano.

Magonjwa hayo ni goti, kifundo cha mguu, nyonga, kuteguka na kuchanika  nyama.

Njia za kuepuka majeraha

  1. Kila mchezaji, timu, klabu kuzingatia kanuni za afya ambazo msingi wake mkuu ni kuwa na wataalamu waliokidhi vigezo vya taaluma zao hususani mwalimu (kocha) na daktari.

ii. Mtiririko mzuri wa mazoezi kulingana na wakati yaani kipindi cha maandalizi, mashindano na baada ya mashindano.

iii. Mawasiliano ya kiutendaji kati ya mwalimu, daktari na wanamichezo, kuzingatia kanuni za afya michezoni kupitia weledi wa kitabibu.

iv. Matumizi bora ya vifaa vya michezo kulingana na mahitaji ya mchezo husika.

v. Upatikanaji wa huduma ya kwanza ya haraka na sahihi katika maeneo ya viwanja kupitia wataalamu wao na uwepo wa vifaa vinavyokidhi haja.

vi. Ushirikiano mzuri kati ya uongozi, dawati la ufundi na majeruhi katika kuhakikisha afya ya wanamichezo inaangaliwa kwa ukaribu.

vii. Chakula bora kwa wachezaji husaidia kuimarisha mwili na kuujenga kiuanamichezo na hivyo huepusha majeraha yasiyo ya lazima.

viii. Mazingira mazuri ya viwanja vya mazoezi na mashindano ambapo inajulikana wazi viwanja vibovu ni chanzo cha majeraha kwa wachezaji.

Madhara ya kuchelewa kupata matibabu

  1. Jeraha hugeuka kuwa ugonjwa/tatizo.
  2. Kukaa nje kwa muda mrefu

iii. Kushindwa kupona vema na kujikuta mchezaji anacheza na maumivu au kidonda.

iv. Uwezo wa kiutendaji kupungua kama si kupotea na kuhatarisha ajira yake.

v. Kuisha kiwango na kupoteza dira kwa umri mdogo.

vi. Kupata ulemavu wa kiungo wa maisha.

Mapumziko kwa mchezaji mwenye jeraha

Matuzya anaeleza kuwa muda wa majeruhi kukaa nje ya mchezo husika unategemea aina ya mchezo, aina ya maumivu, ukubwa wa tatizo, jeraha na afya ya mwanamichezo mwenyewe.

“Kuna baadhi ya wanamichezo wanakuwa na historia ya maradhi ya kudumu ya kuzaliwa nayo, kifamilia au maambukizi ambayo yanaweza pia kuwa kigezo cha mwanamichezo kuchelewa kupona mbali na chanzo cha majeraha yake,” anasema Matuzya.

Anasema kawaida kwa kutumia vigezo alivyovitaja awali, mwanamichezo anaweza kukaa nje ya mchezo kuanzia wiki hadi miezi mitatu.

Anasema isipokuwa mara nyingi majeraha yanayomweka mchezaji nje ya uwanja kwa miezi isiyozidi mitatu kwa uangalizi wa kitaalamu ni mivunjiko ya mifupa, michaniko ya misuli, mikatiko ya migeli na mishipa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles