HAWA NDIO KINA BABA WENYE UMRI MDOGO DUNIANI

0
614

SIKU ya kina baba ni maalumu kwa wale ambao pamoja na mambo mengine huwa wakati mzuri wa kutafakari na kujikumbusha wanakotoka kuanzia siku zao za kuzaliwa hadi ile ya ndoa.

Hata hivyo, kwa baba mtoto anayekutana na siku hiyo huwa katikati ya mzigo wa malezi na umri ambao haujakomaa kwa jukumu hilo.

Katika kizazi hiki mila, desturi na tamaduni zimebadilika kwa sababu ya ujio wa sayansi na teknolojia. Kile kilichokuwa kikionekana kutokubalika katika jamii huko nyuma kimekuwa kitu cha kawaida katika zama hizi.

Sasa kuna vitoto, ambavyo ndiyo vinaanza shule na viko chini ya uangalizi wa wazazi, lakini vimeshakuwa baba.

Wafuatao ingawa baadhi majina yamehifadhiwa ni miongoni mwao baba watoto zaidi duniani na nini tunaweza kujifunza kutoka kwao.

 

James Sutton (12) Uingereza

James Sutton alikuwa na miaka 12 tu wakati alipompa mimba rafikiye wa kike Sarah Drinkwater (16) wakazaa watoto mapacha! Wengi walidhani wawili hao watashindwa kuhimili mimba na maisha kutokana na umri wao. Lakini miaka minane baadaye ikashuhudia wawili hao wakianza maisha ya ndoa na hadi sasa wanaishi kama mume na mke na watoto wao mapacha na binti mwingine waliyemzaa baadaye.

Wakati James akisikitika kwa kuweka rekodi kama baba mdogo zaidi Uingereza kuzaa mapacha, anajivunia kwa kuweza kuvuka milima na mabonde na kuwashushua wale waliokuwa na wasiwasi wa mwelekeo wao wa baadaye, kwa vile maisha yanawaendea vyema ikiwamo ya kikazi.

 

Mvulana wa miaka 12 Urusi

Ilikuwa Julai 12, 2010 wakati mvulana mwenye miaka 12 alipoukwaa ubaba kwa kumzalisha msichana mdogo anayeishi Kazan, Urusi. Msichana alikuwa na miaka 10 tu na alivunja ungo kabla ya kufikisha umri huo.

Mvulana wa miaka 13 Ubelgiji

Mvulana huyu jina linahifadhiwa akiwa na miaka 13 alikuwa baba baada ya kumzalisha rafiki yake wa kike mwaka 2006 aitwaye Montigny-le-Tilleul. Wawili hao walisoma shule moja na mimba ilibainika kwa mama wa msichana kubaini uzito wa binti ukiongezeka. Akamuanzishia  mlo wa kupunguza uzito, lakini halikusaidia na hivyo hospitali ikafichua mimba.

Alfie Patten (13) Uingereza

Alikuwa baba katika umri wa miaka 13 kwa rafikiye wa kike Chantelle Steadman wakipata mtoto Maisie Roxane. Uso wake wa kitoto haukuonesha kana kweli hilo linawezekana na aliwashangaza wengi nchini Uingereza. Hata hivyo ikaja julikana kupitia kipimo cha DNA kuwa si baba halisi bali wa mtoto huyo bali Tyler Barker aliyekuwa na miaka 14.

Mvulana wa miaka  12 Zimbabwe

Baba ambaye hafahamiki alizaa na msichana Samantha Goodman, ambaye alikuwa na umri wa miaka 10 wakati walipoonana. Miaka sita baadaye msichana huyo alifichua kuwa ulikuwa mchezo wa ‘kujificha na kutafutana’ uliosababisha hilo mwaka 2003. Watoto hao wakiwa wamejificha waliona picha ya watu wanaofanya tendo la ndoa hivyo na wao walijaribu kuiga. Msichana hakubaini chochote had miezi michache badaye mamaye yake akawa na wasiwasi na mabadiliko ya mwili na hivyo hospitali ikafichua mimba.

Baba wa miaka 13 Urusi

Baba huyu dogo pia jina limehifadhiwa akiwa na miaka 13 alimbaka jirani yake Anna”Anya” ambaye alikuwa na umri wa miaka minane. Baadhi wanaweza kushangaa inakuaje msichana wa miaka minane akapata mimba kwa sababu msichana huvunja ungo akiwa na umri wa miaka 11 au zaidi. Anya alivunja ungo akiwa na miaka saba akazaa huko Rostov-on-Don Aprili 2000.

Mvulana wa miaka 13 Uingereza

Ni penzi lingine lililotokana na hisia nzito zisizozulika baina ya mvulana wa miaka 13 na msichana wa miaka 12 nchjini Uingereza. Wanahesabiwa kuwa wazazi wadogo kabisa kuwahi kutokea Uingereza, ambao walikutana shule. Watu wanaomjua vyema msichana huyo kamwe wasingeweza kuamini kuwa mwili wake mdogo kiasi kile ungeweza kubeba mtoto wa uzito wa pauni 7.4 sawa na kilo 3.3. Kila mmoja aliyewaona wawili hao alishuhudia uzito wa mapenzi baina yao, kiasi kwamba mara kwa mara wakitamka nia ya kuoana mara mtoto wao atakapozaliwa. Msichana anaishi na mama yake mwenye miaka 27 kaskazini mwa London.

Sean Stewart (12)

Sean Stewart hakuweza kujizuia wakati alipokutana na mama wa mtoto wake wa kwanza Emma wakati akiwa na miaka 11. Emma Webster alikuwa jirani wa familia ya Sean na kitu kikatokea baina yao na baada ya miezi 9 mvulana Sean Stewart akawa baba wa Ben Louis aliyezaliwa Januari 20, 1998 wakati ndiyo alikuwa akifikisha miaka 12.

Sasa akiwa na miaka ya 30 wenzi hao wametengana. Kwa mujibu wa ripoti, Emma anaishi maisha ya furaha na mume mpya wakati Sean amekuwa akiingia na kutoka jela kutokana na wizi. Inatufundisha kuwa si hisia zote nzito za penzi zinatafsiri upendo.

Mvulana wa miaka 9 China

Baba wa miaka 9 nchini China alizaa na msichana wa miaka chini ya 10 nchini China. Imezoeleka nchini China kuwaoana watoto wenya miaka 10 na zaidi wakiolewa pamoja na uwapo wa suala la idadi ya watu nchini humo. Pamoja na sera yake ya kuzaa mtoto mmoja, China bado inaongoza duniani kwa idadi ya watu duniani. Wazazi hao wadogo kwa sasa wana atoto wanne wasichana wawili na wavulana wawili. Hakuna zaidi taarifa kuwahusu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here