29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

HATUA MUHIMU YA UKUAJI KWA WATOTO

MTOTO anapofikisha miaka mitano, asilimia 90 ya ubongo wake inakuwa imeshafanyiwa kitu kinachomaanisha ukuaji wake toka anapozaliwa ambao ni muhimu kwa maisha yake ya baadae.

Ubongo wa mtoto hukua katika hatua tofauti tofauti. Mabadiliko ya ubongo ndani ya tumbo la uzazi, kipindi cha kuzaliwa kuanzia miaka mitatu hadi mitano ni muhimu zaidi kwa watoto wenye afya nzuri ya akili na mwili.

 

Mabadiliko ndani ya tumbo la uzazi

Siku 16 baada ya mimba kutungwa kabla hata hujafahamu kama ni mjamzito, msingi wa ubongo na uti wa mgongo huanza kutengenezwa. Seli za neva huanza kutengenezwa na kufanya ubongo wiki ya 12. Baada ya miezi michache ogani za fahamu na neva huanza kutengenezwa.

Tafiti zinaonyesha matukio yanayotokea yanaweza kuleta athari chanya na hasi kwa ukuaji wa ubongo wa mtoto. Wanawake katika nchi zilizoendelea wanapata fursa ya kumkuza na kumtunza mtoto kabla hata hajazaliwa, tofauti na nchi zinazoendelea.

 

Mabadiliko kuanzia kuzaliwa hadi miaka mitatu

Mtoto kuanzia kuzaliwa hadi miaka mitatu hupitia mabadiliko makubwa ya ukuaji na maendeleo, akitengeneza miunganiko 700 ya fahamu kila sekunde. Mtoto anapozaliwa seli za ubongo bilioni 100 huwa tayari zilishatengenezwa.

Maendeleo ya ubongo wa watoto yapo mikononi mwa wazazi ingawa majirani na ndugu wengine huchangia mno katika maendeleo ya ubongo wa mtoto.

Kuona picha, video na kucheza na midoli humsaidia mtoto kuanza kujifunza kula, kuongea na kucheza kwenye umri wa miaka mitatu.

Asilimia 90 ya maendeleo ya ubongo hutokea kabla ya umri wa miaka mitano. Serikali inapaswa kuanzisha programu za lishe bora na zitakazoweka mazingira rafiki kwa watoto kujifunza na kucheza kwa usalama.

Kulingana na utafiti uliofanywa na wanaanthopojia wa Chuo Kikuu cha Northwestern, mtoto wa miaka mitano anatumia glukosi katika ubongo wake mara mbili zaidi ya mtu mzima. Katika umri wa miaka mitano mtoto hujifunza mengi hivyo ubongo huwa unahitaji nguvu nyingi.

Kwa kuwa miaka ya mapema kuanza shule ni ya mabadiliko makubwa ya ubongo, ni muhimu kundi hili la watoto kupata matunzo mazuri, kupata lishe bora, afya, ulinzi na usalama.

 

Watoto wanaoishi katika hali ya umaskini, sehemu zenye vita na mazingira yote hatarishi wanashindwa kukua vizuri kiakili na kimwili.

Maeneo matano ambayo serikali inapaswa kuyakazia kwa watoto ni pamoja na lishe, afya, michezo, elimu na ulinzi.

Karibia asilimia 20 ya utapiamlo sugu kwa watoto huanza kwa mjamzito aliye na utapiamlo, hivyo mwanamke anaposhika ujauzito anapaswa kutunza vizuri afya yake kwa kuhudhuria kliniki na kupata kinga na chanjo za maradhi mbalimbali. Pia anashauriwa kujifungulia kituo cha kutolea huduma za afya kama ilivyopendekezwa na watoa huduma kipindi cha mahudhurio ya kliniki.

Wazazi wanapaswa kufuatilia ukuaji wa watoto wao kwa kuzingatia umri na kile anachoweza kukifanya mfano mtoto wa miaka mitatu anaweza kugeuka nyuma wakati wa michezo ikiwa hawezi kufanya anachopaswa kukifanya katika umri fulani basi inabidi utoe taarifa kwa wataalamu wa afya.

Ripoti ya Education Commission inadai elimu ya awali inaongeza ushiriki wa watoto katika elimu zinazoendelea. Watoto wanapopata ulinzi wa kutosha wanaweza kukua na kuendelea vizuri kiafya, hisia na akili.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles