27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Hatoturuhusu vurugu uchaguzi Mkuu-Masauni

Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni ameonya watu watakaojaribu kuleta vurugu, wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.

Mpaka sasa mchakato wa uchukuaji fomu za ugombea kwa nafasi za urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, umefunguliwa, huku watia nia kutoka vyama mbalimbali wakiatngaza nia na kwa Tanzania Bara Rais Dk. John Magufuli akichukua fomu hiyo na kwa upande wa Zanzibar tayari makada 15 wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), wakichukua fomu kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais.

Masauni aliyasema hayo jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha ndani na maofisa wa ngazi za juu wa jeshi la polisi visiwani Zanzibar.

Aliwaonya baadhi ya watu watakaojaribu kuvunja sharia, huku akikumbushia katazo la mikutano ya hadhara ya kisiasa mpaka pale ruhusa itakapotolewa na vyombo vyenye mamlaka.

“Amani na utulivu ndio ndio kitu muhimu kwa sasa  kuelekea uchaguzi mkuu, naliagiza jeshi la polisi kushughulika na wote watakaoonekana kujihusisha na matendo yanayoashiria vurugu,tunataka watu watumie haki yao ya kidemokrasia kwa amani na utulivu,mikutano ya kisiasa bado aijaruhusiwa,mamlaka husika zipo na muda ukifika zitaruhusu mikutano  kwa kufuata utaratibu maalumu ambao utazingatia misingi ya amani na utulivu,” alisema.

Akizungumzia uhusiano ya waandishi wa habari na polisi katika kufanya shughuli zao za kihabari, alisema umeandaliwa utaratibu maalumu utakaohusisha wadau wa uchaguzi wakiwepo waandishi wa habari kufanya kazi zao pasina kupata ugumu wowote, huku akisisitiza uhusiano mema kati ya waandishi na polisi yahusishe pia kutoa elimu kwa wananchi kuelekea uchaguzi mkuu.

“Hatutopenda kuona waandishi mnaingia  katika matatizo na jeshi la polisi kipindi cha uchaguzi,tuna utaratibu maalumu utakaowezesha muweze kufanya kazi zenu kwa amani na usalama,hatutopenda kuona matatizo yakitokea kwa waandishi hilo linaenda sambamba na nyie waandishi kufanya kazi na polisi ikiwepo kutoa elimu kuelekea uchaguzi mkuu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles