22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Hatma ya mgogoro wa kitalu  Lake Natron East Hunting kujulikana Aprili, mwaka huu

Na Ramadhan Hassan, Arusha

Hatma ya mgogoro wa kugombea kitalu cha uwindaji wa kitalii cha Lake Natron East Hunting kilichopo Wilayani Longido mkoani Arusha kati ya Kampuni za Kitalii za Green Mile Safaries, Wengert Windrose Safaries na jamii ya kimasai inatarajiwa kujulikana Aprili 15, mwaka huu Jijini Dodoma.

Kitalu hicho kilikuwa kikimilikiwa na Kampuni ya Green Mile Safaries tangu mwaka 2011 ambapo mwaka 2019 aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk.Hamisi Kigwangalla alisitisha leseni ya uwindaji kwa kampuni hiyo kutokana na sababu mbalimbali.

Siku mbili baada ya kusitishiwa leseni mwaka 2019  Kampuni ya Green Mile Safaries ambayo inamilikiwa na Waarabu iliomba marejeo kwa Serikali  ni kwanini imesitishiwa leseni.

Kutokana na hali hiyo, Machi 29, mwaka huu, Waziri wa sasa wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro aliziita Dodoma kampuni hizo ili kutatua mgogoro huo.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii akiwemo Naibu Waziri, Merry Masanja Mkuu wa Wilaya ya Longodo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longodo baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Longido na kila ambaye alitaka kusikiliza.

Mara baada ya Waziri Ndumbaro kutoa nafasi ya kila mmoja kuzungumza aliamuru pande  zote zikutane katika eneo husika ili kuweza kujua tatizo lipo wapi.

AFIKA KATIKA KITALU

Mara baada ya agizo hilo jana Waziri Ndumbaro alifika katika kitalu cha Lake Natron East katika kijiji cha Gedai Lumbwa kilichopo Longido mkoani Arusha na kupokelewa na mamia ya wakazi wa eneo hilo ambao walikuwa wakimsubiri kwa hamu.

Waziri Ndambaro alikuwa ameongozana na Watendaji wa Wizara hiyo pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Ludovic Nduhiye,Mkuu wa Wilaya ya Longodo, Frank Mwaisumbe na baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Longido.

Mara baada ya kufika alikagua mali zilizopo katika kitalu hicho za kampuni ya Green Mile na kuona jinsi zilivyoharibika kutokana na kutokufanya kazi kwa muda mrefu.

Akizungumza na wakazi wa eneo hilo,Waziri Ndumbaro aliwataka kutulia na Serikali itautatua mgogoro huo na majibu watapata tarehe 15 mwezi huu Jijini Dodoma.

“Naomba mtulie majibu yatapatikana tarehe 15 mwezi huu Mkoani Dodoma na baadhi ya watu kutoka huku tutawaalika ili wajue tumeamua nini Serikali yenu ipo na ni sikivu,”alisema Waziri Ndumbaro.

Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa eneo hilo,Mwanasheria wa wakazi hao,Francis Samaito alisema wanaiomba Serikali iifukuzie mbali  kampuni ya Green Mile kutokana na kukiuka  baadhi ya makubaliano waliyoweka na wananchi  ikiwemo kulipa ushuru wa Sh milioni 5.5 kwa kila kijiji.  

“Tunaiomba Serikali iwasikilize hawa wanyonge,wananchi hawana shida na Serikali wanashida na  huyu bwana Green Mile mkataba unaonesha alitakiwa kulipa milioni 329 lakini alilipa milioni 50 pekee nyingine alitokomea nayo,huyu hatumtaki huku kwetu,”alisema.

Naye,Diwani wa Kata Gedai Lumbwa,Saimon Laizer (CCM)  alisema Kampuni ya Green Mile imekuwa haitoi ushirikiano kwa wananchi hivyo wanaomba kitalu hicho kipewe mwekezaji mwingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,205FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles