33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Hatma dhamana ya Kabendera Agosti 5

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imekataa maombi ya Jamhuri ya kutaka kuwasilisha majibu ya kiapo katika maombi ya dhamana ya mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera Agosti 7, mwaka huu.


Jamhuri wamekutana na kikwazo hicho leo Alhamisi saa tatu asubuhi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile anayesikiliza maombi hayo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai maombi hayo yaliwafikia jana na leo shauri linakuja kwa mara ya kwanza hivyo anaomba apewe muda wa kuwasilisha kiapo cha majibu kinzani Agosti 7 mwaka huu kwa sababu kesho atakuwa Mahakama Kuu katika kesi nyingine.


Wakili wa mwombaji, Shilinde Swedy alidai mteja wake yuko chini ya ulinzi kwa zaidi ya saa 24, hajapata uwakilishi wa aina yoyote hivyo aliomba kesi ije Jumatatu.
Hakimu Rwizile alisema kwa kuwa maombi yamekuja chini ya hati ya dharura, muda ulioombwa na Jamhuri ni mrefu, hivyo maombi hayo yatasikilizwa Agosti 5, mwaka huu.


“Maombi yatasikilizwa Agosti 5, mwaka huu siku ya Jumatatu saa saba mchana, wajibu maombi watajibu wakati wowote kabla ya muda huo,” amesema Hakimu Rwizile.
Mwisho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles