28.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

HATIMA YA OLE NANGOLE APRILI 27

Na JANETH MUSHI,-ARUSHA


HATIMA ya kuongezewa muda wa kuwasilisha upya notisi ya maombi ya kukata rufaa ya aliyekuwa Mbunge wa Longido, Onesmo Ole Nangole (Chadema), inatarajiwa kujulikana Aprili 27, mwaka huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Katika maombi hayo namba 18 ya mwaka huu, Ole Nangole alikuwa akiwakilishwa na Wakili Method Kimomogoro na John Materu, huku mjibu maombi ambaye alikuwa mgombea ubunge wa Chama Cha  Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo, Dk. Steven Kiruswa, akiwakilishwa na mawakili Dk.Masumbuko Lamwai, Daudi Haraka na Edmund Ngemela.

Maombi hayo yalikuwa yakisikilizwa na Jaji Sekela Moshi wa Mahakama hiyo ambapo mwishoni mwa wiki  baada ya  mleta maombi kuwasilisha hoja za kuunga mkono maombi hayo na mjibu maombi kuzijibu, alipanga kutoa uamuzi Aprili  27, mwaka huu saa nne asubuhi.

Ole Nangole anaomba  kuongezewa muda kuwasilisha notisi upya ya maombi ya rufaa baada ya ile ya mwanzo kuondolewa pamoja na rufaa, maombi  yanayoungwa mkono na hati ya kiapo cha mleta maombi (Ole Nangole).

Katika hati hiyo ya kiapo, moja ya sababu alizotaja Ole Nangole alidai  alichelewa kuwasilisha maombi hayo akiwa mahakamani anashughulikia rufaa iliyoondolewa mahakamani, ambapo siku 30 baada ya hukumu zilishapita.

Aidha, uamuzi wa Jaji Moshi utaamua iwapo mahakama hiyo imemuongezea muda ili awasilishe notisi na rufaa hiyo katika Mahakama ya Rufaa Tanzania, ambapo wakili Kimomogoro alidai kuwa uamuzi huo ukikataa mteja wake asiongezewe muda watapeleka upya maombi ya rufaa Mahakama ya Rufaa Tanzania au kurudi kwenye uchaguzi.

Awali Februari  23, mwaka huu, Mahakama ya  Rufaa Tanzania, iliondoa kwa gharama rufaa ya Ole Nangole baada ya kushindwa  kuzingatia amri ya mahakama hiyo iliyowataka kufanyia marekebisho rufaa hiyo na badala yake wakaandika rekodi mpya ya  rufaa.

Rufaa hiyo namba 129 ya mwaka 2016, Ole Nangole alikuwa anapinga uamuzi uliotolewa Juni 29, mwaka jana na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, uliomvua ubunge katika kesi ya uchaguzi namba 36 ya Mwaia 2015 iliyofunguliwa na Dk. Kiruswa.

Februari 20, mwaka huu, mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama hiyo, Jaji  Benard Luanda, Jaji  Dk. Musa Kipenka na Jaji Stella Mugasha, rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa ila ilikwama baada ya wakili wa Dk.Kiruswa kuwasilisha pingamizi mbili na kuiomba mahakama hiyo kuondoa rufaa hiyo mahakamani hapo.

Akisoma uamuzi huo jana, Msajili wa Mahakama ya Rufaa nchini, Amiri Msumi, alisema baada ya majaji hao kupitia hoja za kisheria za pande zote mbili kwa kina, wamebaini kwamba mawakili wa mleta rufaa wamekiuka maagizo ya mahakana ya rufaa yaliyowataka kufanya marekebisho na badala yake wakaongeza maneno yao na kuandika rekodi mpya ya rufaa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,099FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles