27.6 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Hatima ya Mrema TLP kujulikana leo

mrmNa Michael Sarungi, Asifiwe George,Dar es Salaam
HATIMA ya Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Agustine Mrema kuendelea kuongoza chama hicho inatarajiwa kujulikana leo baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kuingilia kati.
Hatua hiyo imekuja baada ya kundi la wanachama wa TLP kuandika barua ya malalamiko kutaka kufanyika kwa uchaguzi wa ndani ya chama kwa mujibu wa katiba.
Malalamiko hayo yamemlazimu msajili kuingilia kati na kuziita pande mbili zinazosigana ili kuzungumzia hali hiyo na kutafuta mwafaka kwa amani.
Baada ya malalamiko hayo MTANZANIA ilimtafuta Naibu Msajili wa Vyama, Sisty Nyahoza ambaye alikiri kupokea malalamiko ya sakata hilo, huku akiahidi kutoa ufafanuzi .
“Ni kweli malalamiko yao juu ya mwenyekiti kushindwa kuitisha uchaguzi mkuu Aprili 24, mwaka jana yamefika ofisini kwangu na leo tunatarajiwa kuwa na mazunguzo juu ya hali hiyo,” alisema Nyahoza.
Alisema tayari ofisi yake imeshauandikia uongozi wa chama hicho juu ya kufanya chaguzi ndani ya chama hicho vinginevyo chama hicho kitafutwa.
Alisema chama kiliomba kuahirisha chaguzi ndani kwa sababu ya hali ya kiafya ya mwenyekiti wao, Bunge Maalumu la Katiba pamoja na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ukweli na Maridhiano wa TLP, Joramu Kinanda alisema leo wanatarajia kukutana na naibu msajili wa vyama vya siasa lakini kuna wasiwasi mkubwa kama watatendewa haki.
“Kwa mara ya mwisho chama kilifanya uchaguzi mwaka 2009 na kuhudhuriwa na wajumbe 125 tu kinyume cha katiba,” alisema Kinanda.
Alisema kwa mujibu wa katiba ya TLP wajumbe wanaohitajika ili uchaguzi ufanyike ni 4,200 kitu ambacho hakikufanyika katika uchaguzi uliopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles