31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

HATA KAMA ANAKUPENDA, STORI HIZI ACHANA NAZO KABISA! – 2

KUJIAMINI ndiyo kila kitu katika maisha ya binadamu. Usikubali kukatishwa tamaa wala kuyumbishwa. Simamia unachokiamini.

Hata katika mapenzi, hakikisha unasimama pale ambapo unaamini ni chaguo la moyo wako. Achana na kumfikiria dada, kaka, marafiki au ndugu yako yeyote wakati ukifanya uchaguzi wa mwenzi wa maisha yako.

Wewe ndiye ambaye utaishi naye, mapenzi yako ya dhati ndiyo silaha ya mwisho kabisa kwako. Weka msimamo wako lakini ukiwa na uhakika kabisa kwamba, unautendea haki moyo wako.

Wakati mwingine kunakuwa na ugumu inapotokea wazazi/walezi kutokubaliana na chaguo lako; hapo hupaswi kwenda haraka. Unahitaji utulivu na kuwaelewesha taratibu ili hatimaye waweze kukupa baraka za kwenda kwenye ndoa na mwezi wako.

Marafiki zangu, msingi wa ninachokizungumza katika mada hii ni aina ya uhusiano usiofaa. Kuna mambo ambayo kwa hakika hayana maana katika uhusiano wa mapenzi.

Kuna tatizo la watu kuiga maisha ya watu wengine (hasa kutoka Magharibi), hilo limekuwa tatizo kubwa sana kwa jamii yetu ya sasa.

Wiki iliyopita nilianza kwa kueleza tabia ya baadhi ya watu kuchangamkia mapenzi yasiyokubalika. Kinyume na maumbile. Nilielezea kwa kirefu sana athari zake kisaikolojia na kiafya  na bila shaka kuna mambo ambayo ulijifunza.

Kama wiki iliyopita hukupata bahati ya kusoma ukurasa huu, nataka kukuhakikishia kwamba kuna madhara makubwa sana ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Ukiachia mbali suala la kulegea kwa misuli na kukauka kwa mafuta maalumu ya kulainisha njia ya haja kubwa hivyo kusababisha michubuko, maumivu na hatimaye choo kutoka bila breki, pia kuna tatizo la uzazi.

Wakati wa kujifungua, mwanamke anayeendekeza mchezo huo hatari hukosa uwezo wa kumsukuma mtoto; aibu yote ya nini? Kwa nini uingie kwenye tatizo ambalo unaweza kuliepuka?

 

USAGAJI

Ni jambo la kushangaza sana, siku hizi tabia hii imeota mizizi sana katika jamii yetu. Hivi karibuni, nikiwa nimetembelea ukurasa wangu katika Mtandao wa Kijamii wa Facebook nilikutana na dada mmoja (hapa nafificha jina lake) ambaye aliniomba sana niingie kwenye sehemu za kupokea ujumbe wa pembeni ‘inbox’ ndani ya ukurasa huo kwa vile alinitumia ujumbe wenye shida muhimu.

Ni msichana mwenye umri wa miaka 20, mwanachuo. Alisema mapenzi yamempa mateso kwa muda mrefu sana, wanaume wamekuwa wakimchezea na kumuacha hivyo anajisikia hana hamu ya kuwa kwenye uhusiano (akiwa na umri wa miaka 20 tu!).

Katika maelezo yake, anasema hivi karibuni akiwa likizo nyumbani kwao, kuna mmoja wa jirani na kwao anamsumbua sana kimapenzi.

Anasema: “Yaani utafikiri mwanaume kwa namna anavyoning’a-ng’aniza. Ni mstaarabu kwa kumwangalia, lakini ndiyo hivyo ni msagaji na ameniambia atanipa raha hadi nitashangaa. Nipo njia panda kaka yangu, naomba msaada wako.”

Nilishtuka sana, lakini cha kushangaza zaidi ni kwamba si kwamba hataki ila anaomba ushauri huku akionekana kuwa anaweza kupata pumziko kupitia kwa mwanamke mwenzake (hapo nilihisi huenda alishawahi kufanya mchezo huo).

Ndugu zangu, mapenzi yapo maalum kwa ajili ya mwanaume na mwanamke, si sahihi hata kidogo kwa wanawake kuwa na uhusiano. Athari zake ni nyingi sana, lakini kubwa zaidi ni kupoteza mhemko/hamu ya kuwa na mwanaume.

Hata kama baadaye muathirika akiamua kuacha, hatafurahia tendo na mwanamke wake.

 

USHOGA

Hapa ni wanaume kwa wanaume. Mchezo wao unafanana kidogo na wanawake kwa wanawake. Tofauti hapa ni kwamba, mwanaume mmoja huwa kama mwanamke! Siku hizi kuna ambao hawaogopi hata kidogo kufanya mchezo huu.

Kimsingi ni mchezo hatari sana ambao athari zake zinafanana na zile nilizoanisha kwenye kipengele cha mapenzi kinyume na maumbile. Hata kama umeshaanza mchezo huu, ukiwahi katika vituo vya afya ukaonana na wataalam au washauri, wanaweza kukusaidia kuacha na kuanza ukurasa mpya.

Ndugu zangu, tuachane na mambo ya kuiga, tufuate utaratibu unaofaa kwa kuzingatia maadili yetu Watanzania. Naamini somo limeeleweka.

Hadi wiki ijayo kwa mada nyingine, USIKOSE!

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles