30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Hasunga wataka vijana kugeukia sekta ya kilimo

Na Mwandishi wetu -Songwe

MBUNGE wa Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga,  anakusudia kuwakutanisha vijana kwa ajili ya kongamano la kujadili fursa zilizopo katika sekta ya Kilimo.

Waziri Hasunga ameyasema juzi  wakati akizungumza na vijana wa Jimbo la Vwawa katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa CCM wilayani Mbozi.

Alisema kuwa zaidi ya asilimia 70 ya watanzania wanajihusisha na kilimo lakini miongoni mwao vijana ni wachache. Hivyo,  mkakati huo wa kuwakutanisha vijana ni sehemu ya kueleza kwa vijana fursa zilizopo kwenye sekta ya Kilimo na kuziendeleza.

Alisema kuwa vijana ndio nguvu kazi ya taifa hivyo kuhusishwa kwenye sekta ya kilimo ni miongoni mwa mambo ya msingi yatakayoinua uchumi wa vijana nchini kadhalika kuimarisha uchumi wa Taifa.

Alisema vijana wengi wamekuwa wakijihusisha na mambo yasiyokuwa na tija katika Jamii kama vile kushinda vijiweni badala yake wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuimarisha kipato chao kitakachopelekea vijana kutojihusisha na uovu wa aina yoyote.

Kuhusu kuimarisha masoko ya mazao mbalimbali ikiwemo zao la kahawa, alisema kuwa tayari wizara ya kilimo imeanzisha mkakati kabambe wa kuongeza minada ya kahawa ambapo kwa upande wa Kanda ya ziwa mnada utafanyika mkoani Kagera, Kanda ya Kaskazini utafanyika Manispaa ya Moshi, Kanda ya kusini utafanyika wilayani Mbinga na Kanda ya nyanda za juu kusini mnada wa kahawa utafanyika Wilayani Mbozi.

Aliongeza kwamba kuongeza minada ya uuzaji wa zao la kahawa utatoa fursa kwa wakulima kunufaika na mazao yao kwa kuuza kwa bei nzuri na kulipwa kwa wakati.

“Kumekuwa na mbegu nyingi mtaani ambazo sio sahihi kwa maana hiyo sasa serikali inachukua hatua kali kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara hiyo punde watakapobainika,” alisema Hasunga

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,195FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles