28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Hasunga awataka wapiga kura waweze kujikinga na corona

Mwandishi Wetu -Songwe

MBUNGE wa Vwawa ambaye ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga ametoa salamu za pole kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk Ayub Rioba, familia nzima ya televisheni hiyo na wafiwa wote kwa misiba ya wanahabari wake.

Salamu hizo alizitoa juzi mbele ya waumini wa kanisa la Last Church lililopo Mjini Vwawa mkoani Songwe wakati wa ibada ya Pasaka .

Waziri Hasunga alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha viongozi wa dini na waumini wote nchini kujikinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya corona wakati wakiwa katika ibada na kwenye shughuli zao za kila siku.

Waziri Hasunga amewataka Watanzania wote kwa pamoja kutambua kuwa ugonjwa huo ni janga la dunia nzima lisilobagua matajiri wala masiki hivyo muhimu kila mmoja kuchukua tahadhari iwezekanavyo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles