30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Hasunga ataka Watanzania kunywa kahawa kwa wingi

Na Mwandishi wetu-Kagera

WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga, amesema Mkoa  wa Kagera ni miongoni mwa mikoa inayozalisha zao la kahawa kwa wingi nchini, lakini wananchi wa mkoa huo hawana utamaduni wa kunywa kahawa wanayoilima.

Hasunga alisema alipofanya ziara katika kiwanda cha kahawa cha AMIMZA kilichopo Halmashauri ya Wilaya Bukoba mkoani humo.

“Wananchi wa Bukoba pamoja na Watanzania kwa ujumla wake kama wangeweza kutumia ipasavyo kahawa yao tusingekuwa na tatizo la masoko ya kahawa, hivyo nawasihi wananchi wenzangu kuhakikisha mnatumia kahawa ipasavyo ili kuimarisha soko letu la ndani” alisema Hasunga.

Hasunga aliongeza kuwa kahawa inayolimwa Kagera imekuwa bora duniani na baadhi ya kampuni huitumia kwa kuiwekea lebo nyingine na kunufaika zaidi.

“Naona ipo haja ya watu wetu kuelimishwa faida za unywaji wa kahawa. Lakini nawapongeza sana kwa uwekezaji mkubwa mlioufanya hapa Kagera,” alisema  Hasunga.

Alisema Mkoa wa Kagera unafursa nyingi za uwekezaji hasa za viwanda na kuwasihi wawekezaji kujitokeza kwa kuwa usalama ni wa kutosha na kwamba kahawa inatakiwa kuwa zao bora nchini.

Kwa niaba ya mmiliki wa kiwanda cha AMIMZA,  Billal Amir Hamza alisema kiwanda hicho kipo katika maboresho kwa kuongezea baadhi ya idara na kikikamilika kitaweza kutoa ajira kwa Watanzania 600.

Alisema kiwanda kikikamilika kitaweza kuzalisha kahawa mumunyifu (Instant) tani 6,000 sawa na tani 18,000 za kahawa safi ambazo ni sawa na tani 36,000 za kahawa ya maganda.

“Hadi sasa pamoja na uzalishaji unaoendelea, tumeajiri wafanyakazi 59  na kutoa ajira nyingine kwa wananchi ambao ni majirani zetu hapa, tumejenga kiwanda kikubwa Africa Mashariki na kati, niseme tu sisi soko letu lipo nje ya nchi ila kwasasa tumerudi nyuma baada ya janga hili la Covid-19 ,” alisema Billal.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles